Serikali itangaze dau ili kupata suluhu katika maboresho ya usalama wa bodaboda

Serikali itangaze dau ili kupata suluhu katika maboresho ya usalama wa bodaboda

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
Lema aliibua hoja ya msingi sana ambayo wahuni wameifunika katika propaganda nyepesi kwamba alisema kazi ya bodaboda ni laana.

Hilo ni kwa mtazamo wake, lakini kwa upande wangu mimi siwezi kuiita laana maana inalisha familia za watu, kusomesha na kujenga, ni ajira kama ajira nyingine.

Naishauri serikali itangaze dau vijana watoe mawazo yao ya ubunifu, tutapata namna bora ya kupunguza ajali na maafa mengine yatokanayo na bodaboda kwa kiasi kikubwa. Wasijifiche katika propaganda na kuacha hoja ya msingi.

Hakuna cha bure.
 
Hii Mada ni Pana sana.kwa sasa utaona hata bei ya vyakula ipo juu hii ni kutokana na vijana wenye nguvu kushinda stend wakisubiri abiria.
Wazee ndio huenda Mashambani kulima na kuzalisha chakula.Bei ya vyakula itazidi kuwa juu.
 
kwamba bodaboda zipigwe marufuku vijana wakalime?
 
kwamba bodaboda zipigwe marufuku vijana wakalime?
Hapana wazo ni kuwa,bei ya pembejeo ishuke Ili kuwavutia vijana wakalime.

Kwa Hali ya pembejeo sasa vijana wanaona Bora Boda Boda na bajaji au guta.
 
Hapana wazo ni kuwa,bei ya pembejeo ishuke Ili kuwavutia vijana wakalime.

Kwa Hali ya pembejeo sasa vijana wanaona Bora Boda Boda na bajaji au guta.
Tujadili hoja ya msingi sasa,je Bodaboda ni laana ama si laana,na kwa nini ni laana kama ni laana? ,nini kifanyike kuondoa kile kinachoifanya iwe ya laana?
 
Back
Top Bottom