Serikali itasimamia na kutekeleza matakwa ya wananchi katika kupata Katiba mpya

Serikali itasimamia na kutekeleza matakwa ya wananchi katika kupata Katiba mpya

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
Na Miza Kona-Maelezo Zanzibar

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeendelea na msimamo wake wa kuwahahakikishia Wazanzibari kuwa itasimamia na kuyatekeleza matakwa yao watayokubaliana katika Mabaraza ya Katiba ili kupata Katiba Mpya yenye kukidhi mahitaji yao.

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Abubakar Khamis Bakary ameyasema hayo wakati akisoma hotuba ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara yake mwaka wa fedha 2013/2014 Katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Amesema jambo la msingi kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni kufanya maamuzi ya kujua wanataka Muungano wa aina gani na Katiba ipi ili Wananchi watakapoenda kutoa Maoni yao katika Mabaraza ya Katiba wawe na hoja za msingi.

“Kwanza ni sisi wenyewe kujua tunataka Muungano upi na Katiba ipi kasha tuwaelimishe wananchi wetu”Alisema Waziri Bakary.

Amesema Wanachi wasiwe na wasiwasi na kwamba kupitia kwa Wawakilishi wao waijadili Rasimu ya Katiba na kuona kama inakidhi haja ya kuleta Maendeleo, Maisha mazuri na haki za Wazanzibar kwa kizazi kilichopo na kijacho.

“Tuhakikishe kuwa Katiba ijayo inafufua matarajio ya Wazanzibari kwa Zanzibar yetu ya leo na siku za usoni”alisema Waziri Bakary

Aidha Waziri Bakary ameitaka jamii kufahamu kuwa Katiba inayotakiwa itabadilisha sana Taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii na kwamba Wananchi wanatakiwa kuwa imara na mazingatio ya mabadiliko hayo.
Alieleza kuwa mabadiliko yatakayotokana na Katiba Mpya yanaweza kuwa ya karibuni na mengine kuchukua muda mrefu hivyo wananchi wajitayarishe kukabiliana nayo

Katika hatua nyingine Waziri Bakary amesema Wizara yake kupitia Idara ya Mahkama imepanga kupunguza mrundikano wa kesi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa haki.

Aidha Majengo ya Mahkama ya Unguja na Pemba yanatarajiwa kufanyiwa matengenezo ili kuyapa hadhi ya kisasa.

Katika kutekeleza majukumu yake Waziri huyo ameliomba Baraza la Wawakilishi limuidhinishe jumla ya sh. 8,188,000,000.00 kwa matumizi ya kazi za kawaida.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
 
Naona kuna kitu kina kosekana hapo... Mbona hakusema ukweli tu pia waamue kama wanataka muungano au la!!!
 
wanachokitaka wameshakisema zamani ila tume ya watanganyika wanalazimisha muungano,,, alichosema waziri ni kuwa watasimamia maamuzi ya wananchi hii ina maana kupitia maamuzi ya kura,, Wazanzibari sio wanafiki ila watu wanaojiita watanzania bara manake hata kutaja jina la nchi yao wanaona aibu kutokana na kuzidiwa na utumwa wa akili.
 
Back
Top Bottom