kiongozi wa masikini
New Member
- Oct 29, 2024
- 2
- 2
Serikali inapambana sana kusaidia wananchi wapate HATI zao kwa wakati. Wizara ya Ardhi imekuwa mstari wa mbele sana kuhakikisha kilio cha HATI kinaisha, na tumekuwa mashahidi kwa sasa serikali imeongeza kasi kubwa sana kuhakikisha watu wanapata hati zao. Awamu hii ya sita imekuwa mstari wa mbele sana kutoa Hati kwa wakati, na juzi tumeona Mkuu wa mkoa wa Dar alifanya ziara usiku wizara ya Ardhi na kupokelewa na Katibu Mkuu. Tumeona Hati zinatolewa hadi usiku (usiku wa manane)!
Ila moja ya watu wanaokwamisha juhudi hizi ni MSAJILI. Huu ni mwezi wa nne, hadi sasa tunaangaika na msajili apitishe hati zetu, ila imeshindikana. Kauli anazotoa siyo nzuri; kupitisha file tupate nambari ya malipo (control number) ni kitendo cha muda mfupi, hata dakika moja haifiki, ila ni miezi sasa file limekwama kwa msajili.
Tunamuomba waziri wa wizara husika, sisi ni wale tumekosa ajira, tumejiajiri, tumepambana, tumejenga, tumeingia katika mikopo bank na tunategemea hii mikopo kuendesha maisha. Hadi sasa mikopo yetu haijakamilika, tunasubiri hati ili bank ipitishe mikopo yetu; ni miezi sasa tumekwama. Kauli ya mwisho ya Msajili alisema TUSIMFUNDISHE KAZI, hadi leo hatujui ni lini msajili atapitisha haya mafaili. TEGEMEO LETU LA MWISHO NI HII POST!
SERIKALI TUNAOMBA ANGALIENI HILI SUALA KWA UNYETI SANA OFISI YA MSAJILI HAPO DAR ES SALAAM. Watu wamekwama; moja ya mtu aliekwama ni hawa wanaosubiri msajili apitishe hati zao wakachukue mkopo wampeleke mzazi wao katika matibabu nje! Wote sisi tumekwama; serikali TUNAOMBA SANA MTUSAIDIE KATIKA HILI!
Wizara ya Ardhi