ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
Chama cha ACT Wazalendo inaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa taarifa rasmi kuhusu hali ya usalama ya wanajeshi wetu walioko katika operesheni za kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Hii inafuatia taarifa za hivi karibuni za kuongezeka kwa mashambulizi ya waasi wa M23, ambao wameingia na kudhibiti mji wa Goma na mashariki mwa DRC.
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, mapigano haya yamesababisha vifo na majeruhi kwa mamia ya raia na baadhi ya wanajeshi kutoka vikosi vya kulinda amani kupitia Umoja wa Mataifa (MONUSCO) na SADC (SAMIDRC). Nchi kama vile Afrika Kusini imeweka wazi wanajeshi wake waliopoteza maisha wamefikia 9, Malawi 3, Botswana 5 na vingine.
Hali hii imezua wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa vikosi vyetu vilivyoko katika maeneo hayo yenye machafuko.
Tunatambua na kuthamini mchango wa wanajeshi wetu katika kudumisha amani na usalama barani Afrika. Hata hivyo, tunashangazwa na ukimya wa Serikali ya Tanzania kuwajulisha wananchi juu ya hali ya usalama ya wanajeshi wetu na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha usalama wao katika mazingira haya hatarishi.
ACT Wazalendo tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua zifuatazo;
i. Kuwajulisha wananchi kuhusu hali ya usalama ya wanajeshi wetu walioko DRC na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha usalama wao.
ii. Kuhakikisha kuwa wanajeshi wetu wanapata vifaa na msaada unaohitajika ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na usalama.
iii. Kufanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa ili kuhakikisha kuwa amani inarejeshwa haraka katika maeneo yaliyoathirika na machafuko
Mwisho, ni wakati wa Tanzania kutathmini upya msimamo wake wa kushiriki kutuma vikosi ambavyo haviondoi mzizi wa mzozo huu. Vita hivi vinasababishwa na maslahi ya kiuchumi na unyonyaji wa rasilimali za Kongo unaofanywa na makundi ya maslahi na mataifa ya kibepari. Tunapaswa kuweka msisitizo katika kulinda utu na kusimamia haki za watu wa Kongo badala ya kuwa sehemu ya mzunguko huu wa machafuko yanayonufaisha wachache.
Imetolewa na;
Ndg. John Patrick Mbozu
Waziri Kivuli wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Januari 28, 2025