Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Bila jitihada za serikali kuweka msisitizo wa kuzuia au kupunguza adhabu ya viboko mashuleni; kuna uwezekano mkubwa wa kuzalisha taifa lenye walemavu wengi!
Binafsi niliwahi kuchapwa enzi hizo nikiwa sekondari kwa kosa la jumla (darasa zima) na walimu karibu 10 kwa wakati mmoja. Nilipata maumivu ya kidole ambayo hadi leo hii kuna wakati kidole hicho huuma!
Hapa miaka ya katikati (wakati wa JK) Adhabu ya viboko ilipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na kampeni ya 'shule rafiki'
Kwa sasa adhabu hii imeshika kasi sana. Wanafunzi wanachapwa kuliko idadi inayotakiwa. Sababu zipo nyingi (kwa mtazamo wangu) ambazo zianweza kuwa:-
•Idadi kubwa ya wanafunzi isiyoendana na idadi ya walimu husika.
•Maslahi duni ya walimu.
•Uwezo mdogo wa kitaaluma/kitaalam kwa baadhi ya walimu na hivyo wanaona viboko ndio njia pekee ya kumfanya mwanafunzi aelewe.
•Majukumu mengi kwa walimu (kuamua kesi za wanafunzi za kupigana, kuibiana nk, kuwa washauri nasaha, kudhibiti nidhamu nk nk)
•mmonyoko mkubwa wa maadili katika jamii. Watoto wengi wanajilea wenyewe kutokana na baadhi ya wazazi kuwa 'busy' kutafuta kipato au kulelewa na wasaidizi wa kazi za nyumbani na hivyo kusababisha kukosa maadili stahiki.
Kuna uwezekano mkubwa walimu wengi hawako sawa kisaikolojia. Kwasababu binadamu aliye sawa hawezi kumuadhibu binadamu mwenzako kiasi cha kumjeruhi. Serikali iingilie kati. Wanafunzi watazidi kuwa wakatili kutokana na ukatili wanaofanyiwa wao katika umri mdogo!