KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Mimi ni mmoja wa Wakulima wa mahindi, kwa kawaida baada ya kuvuna Wakulima wengi huwa tunauza mazao hayo kwa Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).
Tangu Wakulima tuuze mazao yetu kwa Serikali mwezi Septemba 2024 mpaka sasa tunaelekea katikati ya Desemba 2024 hatujalipwa malipo yetu ya kuuza mazao ilhali walisema malipo watatupa ndani ya siku 14 tu tangu tulipowauzia.
Kiukweli tunateseka sana, maana msimu wa kuandaa mashamba umefika na msimu wa kununua pembejeo ndio unaisha.
Hii changamoto imetukumba sisi wakulima wa huku Rukwa pamoja na Mkoa wa Songwe.
Kutokulipwa pesa zetu kwa wakati kumesababisha tuanze kufilisika na turudi nyuma kisa tu tuliiamini Serikali, baadhi yetu wameanza kutumia mitaji waliyonayo katika matumizi binafsi kwa kuwa hatuna fedha ya kuendelea shughuli zetu.
Tunataka Serikali itulipe pesa zetu kama tulivyokubaliana.
Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa wataanza kutulipa na wengine wanasema kuwa wanalipa kidogokidogo, lakini mbona hawaweki wazi, maana tukiwatafuta wahusika wanaishia kusema fedha hazitoshi.
Pia soma ~ RC Chongolo: Malipo ya Wakulima kutoka NRFA yamechelewa kidogo, Waziri amenihakikishia watalipwa