UTANGULIZI
Shirika la posta nchini kwa miaka mingi toka kuanzishwa kwake limekua na huduma za kusua sua huku kazi ya Usafirishaji vifurushi ikitawaliwa na Sekta binafsi huku Serikali ikipoteza mapato mengi katika eneo hilo wakati huo huo wananchi wengi wakitumia gharama kubwa kupata huduma hizo pamoja na kupata usumbufu mkubwa wakati mwingine kwa vifurushi na mizigo yao kupotea au kuharibika wakati wa usafirishwaji kutokana na kutumia njia binafsi zisizo rafiki mfano malori mabasi nk.
Shirika la posta limeendelea kuwa dhaifu kiutendaji huku Serikali ikilazimika kulihudumia wakati lilikuwa linao uwezo mkubwa kujitegemea na kutoa gawio kubwa kwa Serikali hasa ikizingatiwa huduma za posta ni hitaji la kila siku la wananchi.
Nini kifanyike kuboresha Shirika hili labposta na kuwarahishia huduma ^wananchi? Nashauri yafuatayo yafanyike:
1. Shirika la posta nchini liwe na one stop center maeneo yote ya kimkakati mfano njia panda za mikoa na wilaya kama Nzega mkoani Tabora Manyoni Mkoani Singida, Chalinze mkoani Pwani, Mwigumbi mkoani Shinyanga; pia katika makao makuu ya miji yote midogo na mikubwa mfano majiji, wilaya na Manispaa. Maeneo mengi nchini hususan nje ya miji hupata changamoto kubwa mno Kwenye kusafirisha vifurushi vyao kwenda maeneo mbalimbali nchini hivyo kuwapa wakati mgumu katika uratibu wa vifurushi hivyo mpaka kufika kwake kwa walengwa.
2. Kila center moja iwe na Watumishi angalau wawili, mtu wa kumbukumbu na mtu wa hesabu (mhasibu) hii itasaidia kupunguza utitiri wa Watumishi kujikusanya sehemu moja bila tija ambapo kwa sasa wote wapo ofisi ya posta mkoa. Watumishi hao wafanye kazi kidigitali kwa kufanya malipo katika mifumo ya kielekroniki kuepusha rushwa, wizi na upotevu wa mapato ya serikali. Kila mteja atakapolipia kifurushi kwenye control number watakayo mpatia apewe nakala ya risiti ya kielekroniki kama ushahidi wake na dhamana ya mzigo au kifurushi chake pia mteja apewe namba ya Mawasiliano kwa ajili ya kufuatilia mrejesho wa kifurushi chake ambapo Wataalamu wa one stop center watakua na jukumu pia la kufanya Mawasiliano na wenzao kuhusu mwenendo wa vifurushi husika.
3. Shirika la posta lisaini mkataba wa utendaji (MoU) na mashirika na taasisi zote za Serikali chini ya Makubaliano ya vifurushi vyote vya taasisi husika kusafirishwa bure ila magari ya taasisi husika zote yapite hizo one stop center za Shirika la posta kila yawapo safarini kila siku na kupewa vifurushi vya kusogeza center zinazofuata kulingana na safari zao ambapo hili litafanikiwa mno kutokana na kwamba magari ya serikali na taasisi yanasafiri kila siku kuelekea maeneo tofauti tofauti na yana nafasi zinaenda tupu za kuweza kubeba vifurushi.
Hii itasaidia Shirika kuokoa fedha nyingi sana za Usafirishaji vifurushi na rasilimali ya mafuta ya serikali kutumika kwa ufanisi mkubwa kwakua magari yite ya serikali kila yanaposafiri hata bila vifurushi mafuta lazima yatumike vile vile kila siku.
Shirika likikusanya vifurushi vile ambavyo havisafirishiki kwa gari za Serikali eneo husika Wataalamu hao wa one stop center wawe na kibali cha kukodisha au kulipia vifurushi husika kwa wasafirishaji binafsi. Baadhi ya mashirika na taasisi ambazo Shirika la posta litanufaika mno na mkataba huo wa utendaji kazi nk Shirika lq Reli TRC, Shirika la ndege nchini na taasisi zote za Serikali na halmashauri nchini. Taasisi zote za Serikali zipewe muongozo huo wa usafirishaji vifurushi na madereva wote wa gari za Serikali wazingatie muongozo huo na kutambua one stop center zote za Shirika la posta kila wapitapo na kupokea vifurushi. Kila dereva awe anasaini logbook inayoonesha namba ya gari, taasisi, jina, saini na aina ya kifurushi alichopokea kwenye one stop center husika na anapopeleka asaini Vivyo hivyo Kwenye one stop center anayoenda kukabidhi vifurushi husika na kuendelea na safari au shughuli zake nyingine eneo husika.
4. Shirika la posta lipunguze gharama ya Usafirishaji vifurushi kwa angalau 30% kulinganisha na ile inayotolewa na Sekta binafsi ili kuwavutia zaidi wateja na kuongeza mapato kwa Serikali sambamba na kupunguza gharama ya huduma hiyo nyeti kwa wananchi na kuwapunguzia kero ya kupoteza vifurushi, ucheleweshaji wa vifurushi na kuharibika vifurushi vyao katika Usafirishaji.
5. Matangazo ya huduma za Shirika la posta nchini yatangazwe kwa ofa kwenye vyombo vya habari chini ya Makubaliano ya MoU pia, Shirika hilo liweke Mpango wa kufanya navyo kazi kwq ushirikiano ili kuongeza tija na ufahamu kwa wananchi. Hadi sasa Shirika la posta nchini lipo nyuma sana kwenye kujitangaza na utoaji wa huduma zake upo kienyeji sana sio kidigitali.
Nawasilisha.

Upvote
1