SERIKALI ITUMIE RASLIMALI ZAKE VIZURI KWA AJILI YA UOKOZI

MaweSaba

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2024
Posts
416
Reaction score
641
Maisha ya Mtanzania yana thamani gani?
Ni swali najiuliza kila siku linapokuja maswala ya majanga hapa nchini ya maji, moto, ajali za barabarani na mengineyo.

Ajali ya ghorofa kaiakoo, ilichukua wiki kufanya zoezi la uokozi
Meli kuzama Zanzibar na Lake Victoria mpaka leo bado kuna uzembe/ucheleweshwaji unaogharimu maisha ya watanzania, mfano Ndege ya Precision au MV Bukoba.

Nina wazo

Katika kila majiji, serikali iweke vikosi vitatu vya dharura, FIRE, POLISI, AMBULANCE standby. Hawa wawepo kila kilometer tano kwenye barabara kuu zote au makutano, wawe tayari kuokoa maisha ya watanzania muda wote
Boti za uokozi ziwepo doria kwenye maziwa na bahari ili itokeapo changamoto uokozi ufanyike haraka.

Wakati wa maandamano tuliona juhudi za kulinda amani muda wote, basi wawepo pia kwa ajili ya kazi ya uokozi muda wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…