Serikali itunge sheria kali kwa watakaoharibu uwanja wa Taifa ili iwe fundisho kwa wengine

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Gharama zinazotumika kukarabati uwanja wa mkapa kwa ajili ya mechi ya ufunguzi baina ya mnyama vs Al Alhy zingeweza kujenga madarasa au kununua madawa hospitalini au kujenga zahanati hata 30 lakini zimepelekwa pale kwa mkapa.

Kuna wajinga huwa sio binadamu wa kawaida, siku ya ufunguzi watakwenda vyooni kuharibu masinki, kuna watakaoharibu mazingira vyooni kwa makusudi, kuna watu watakanyaga viti ali mradi tu uwanja uharibike.

Ushauri wangu kwa serikali.

1. Elimu itolewe kwenye vyombo vyote vya habari kuhusu umuhimu wa kuutunza uwanja huo.

2.Kamera zifungwe hadi vyooni ili wachafuzi na waharibu mazingira wabainike

3.Sheria itungwe ili kwa atakayebainika adhabu kali ichukuliwe dhidi yake.
 
Cha kushangaza kuna timu mechi ya ufunguzi wakipewa nafasi eti walinde uwanja wanakwenda ku uchimba ili wafukie makafara.
Tangu lini uwanja ukalindwa, kwani kuna atakayekuja ku uiba!!!
 
Hizo Gharama ni za watz wenyewe....una haki ganii ya kuwashitaki
Cha msingi ni watu wa Tanzania wajitambue tu
 
1. Uwanja Gani???
Uwanja wa TAIFA wa ndege???????

2. Nani anayeharibu uwanja?????

3. Huwa wanaharibu uwanja au maeneo ya uwanja????

4. HAO security wanakuwa wapi????

AKILI NI MALI
 
Shida ni umasikini.
Wewe na hela zako ukang'oe koki za mabomba na kuharibu sinki kweli?
Serikali inabidi ifanye njia za kupunguza majobless
  • Waruhusu matumizi ya kupokea na kutuma pesa kwa paypal. Itasaidia kuongeza mzunguko wa hela na watu kujiajiri
  • Washushe gharama za bando na pia waruhusu Starlink. Itafanya watu wasiwe na msongo wa mawazo
  • Watoe ajira kama zamani za walimu na madktari kama zamani 2015 kurudi nyuma walikuwa wanatoa ajira
  • Wapunguze au kuondoa kodi kwenye suala la kianzisha biashara.
 
Na Kuna wengine wataenda kuuchimba uwanja kufukia kondoo zao za makafara ili washinde mechi wasiruhusiwe kufanya ujinga Kama huo na wanajulikana washajipanga kuendeleza upuuzi wao mechi ijayo, washinde kwa uwezo wao na sio nguvu za wachawi wao
 
KICHWA CHA HABARI KILIPASWA KUWA.

SELIKALI ITUNGE SHERIA KALI WATAKAOHARIBU MIUNDOMBINU UWANJA WA BENJAMIN MKAPA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…