Serikali iuenzi Mziki wa Dansi wa zilipendwa wa Tanzania kuwa urithi wa Taifa

Serikali iuenzi Mziki wa Dansi wa zilipendwa wa Tanzania kuwa urithi wa Taifa

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Wizara ya Sanaa, tamaduni na michezo. Hivi mna mawazo Gani kuenzi na kutambua mchango wa mziki wa Dansi na watunzi wake?

Kwa ujumla Muziki wa zamani umechangia sana kukuza utamaduni wa kitanzania na lugha ya kiswahili lakini sijawahi kusikia mikakati ya wizara kuenzi na kutambua mchango wa wazalendo hao kama jabali la Muziki kama Marijani Rajab, Mbaraka mwinshehe, Zahir Ally Zoro,Hemed Maneti, Patric Pama Balisidya, Juma Kilaza, Maestro King Kiki.

Na wengine wengi. Kwa nini kusiwe na Maktaba ya Muziki wa Dansi Ili kuifanya Sanaa idumu vizazi na vizazi. Leo hii Kuna watu hawatambui chimbuko na Historia ya Sanaa ya Muziki wa Tanzania. Serikali Ienzi Historia ya Sanaa hii isipotee.
 
Wazo zuri. Unaandika ukiwa wapi mkuu??...hahah!...weekend hii you know...
 
Kiongo
Makumbele
Shilingi yaua
Monika
Mpenzi ruta
Nikitazama dirishani
Machozi ya samaki
 
Hili ni wazo zuri sana, wanamuziki wa rumba wa zamani walifanya kazi kubwa sana naomba wadau mmoja mmoja nao watoe mchango katika hili. Kwanza kwa wale wanaowajua vizuri basi watoe makala ama hata kitabu juu ya wanamuziki hawa wakongwe ama hata kwa kuelezea walivyojisikia kwa kushiriki katika madansi waliyopiga. Kama zipo picha za madansi hayo ni vyema kuziweka wazi ili tujifunze. Mimi nami ni mpenzi mkubwa wa muziki huu kwa upande wangu nimeamua kuandika kitabu cha mwanamuziki Juma Kilaza na Mbaraka Mwinshehe kwa kuwa nimewafahamu wanamuziki hawa toka utotoni kwa kuhudhuria mazoezi na madansi waliyokuwa wakipiga isitoshe nimefanikiwa kukutana na wanamuziki walioshiriki na nguli hawa na kufanya nao mazungumzo vitabu hivyo vipo katika hatua ya kuchapishwa. Vilevile nimewapa ushirikiano mkubwa Muhataj Mabaraka ili arudie kazi ya baba yake na tayari amesharudia nyimbo nne: Shida, Morogoro yapendeza, Ester, Soniasa na Maneno Kilaza arudie kazi za Juma Kilaza tayari nyimbo Semeni, Zena, Morogoro hoyee and Asha zimerudiwa nyimbo zote hizo zinapatikana youtube. Nimefarijika sana kwa jinsi wimbo SHIDA ulivyopokewa sijui kwa kuwa upo katika video. Naomba wadau wazipokee nyimbo nyingine zote kama walivyofanya kwa wimbo SHIDA. Kwa upande wa serikali nami naunga mkono wazo la kuanzisha jengo la kumbukumbu kwa wasanii hawa
 
Back
Top Bottom