Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Hello!
Nikiwa kwenye corridor za umma takribani miaka 10 sasa nimejionea uzembe wa kiwango kikubwa sana. Watumishi wengi wa umma maadamu mshahara wao ni lazima wapate kila mwezi na posho zipo palepale basi watumishi hawataki usumbufu kabisa. Hata ubunifu hakuna.
Unakuta ofisi leo inaomba taarifa za watumishi kama NAMBA ya NIDA, TIN NUMBER au check number, baada ya miezi 6 unasikia tena ofisi inaomba TIN NUMBER au NAMBA ya NIDA, unaanza kujiuliza hivi ofisi ya ma HR au IT wanafanya kazi gani kama kutunza taarifa jumuishi za watumishi imekuwa kazi kubwa kwao?
Sio ajabu ofisi ya umma imehama mahali miezi 6 imepita lakini ukiingia google map taarifa hazijabalishwa,
Kuna ofisi moja ya umma nilipiga namba yao ya simu akapokea raia wala haijui hiyo ofisi na nilipomuhoji akasema mara nyingi tu hupigiwa simu na watu wakidhani ni namba ya ofisi hiyo ya serikali.
Mambo mengi yako shaghalabaghala, mpaka wasikie wakaguzi wanakuja ndipo kila mtumishi anaanza kusafisha njia yake. Serikali ingeingiza mfumo wa GAIN AS YOU EARN, watumishi walipwe si kwa cheo bali kwa maingizo waliyoyafanya lakini hili naona ni gumu maana kuna taasisi hazifanyi biashara au uzalishaji wowote.
Dawa ni kuunda TAASISI YA USIMAMIZI NA UKAGUZI KWA WATUMISHI WA UMMA.
Kila mkoa iwepo ofisi, watumishi wa taasisi ya USIMAMIZI NA UKAGUZI KWA WATUMISHI WA UMMA watakuwa wanapita kukagua majukumu na utekelezaji wa majukumu kwa watumishi wa umma. Haya mambo ya PEPMIS tunayajaza tunapeana 90% maisha yanakwenda.