Serikali iunde Tume huru ya kuchunguza kifo cha Bw. Robert Mushi maarufu kama Babu G

Duuh
 
Watumishi wa Mochwari wanasema maiti ililetwa na Askari. Walipoulizwa majina ya Askari na wanatoka kituo gani, wamewataka ndugu wa marehemu kuuliza uongozi wa hospitali. Viongozi wa hospitali walipoulizwa wakataka ndugu kuwasiliana na Msemaji wa jeshi la Polisi, kwani wao sio wasemaji.
 

Ukisoma mealezo ya J4 na Malisa yanakinzana....Muliro anasema aligongwa na gari Kimboka ila ndugu wanasema alikamatwa na watu waliojitambulisha kama polisi.

Ndugu walimtafuta hospital na vituo vyote wakamkosa na polisi walisema hawana taarifa zake ila baada ya siku 10 ndiyo wakatoa taarifa yupo mochwari...Ina maana traffic hawadocument ajali zinazotokea barabarani ambazo reported?
 
Ninasikiliza redio eti Muliro anasema marehem aligongwa na gari. Je polisi waliutangazia umma kwamba kuna mtu amegongwa na gari na amefariki? Mambo haya yasikie kwa jirani.
 
Kamanda Muliro aliyemshauri aandike barua ya vitisho Kwa whistle blowers kampoteza maboya.
Taarifa ya kupotea Mushi ilikuwepo Polisi na mitandaoni siku 3 kabla ya April 11 anayosema ndiyo siku waliokota mwili wa Babu G. Picha ilipelekwa Polisi na mitandao zaidi ya 3 ilikuwa na picha yake. Hao Polisi walishindwaje kuutambua mpaka siku 11 baadaye ndugu walipofika Kilwa road Police hospital?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…