Serikali iwasaidie mama lishe kupata majiko na mitungi ya gesi kwa riba nafuu

Serikali iwasaidie mama lishe kupata majiko na mitungi ya gesi kwa riba nafuu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nilimsikiliza Rais katika ufunguzi wa kitu cha mabasi Magufuli kule Mbezi akitambua mchango wa mama lishe katika jamii.

Mama lishe wengi wanatengeneza chakula katika hali ngumu sana. Wengi wanatumia kuni kama nishati ya kupikia, sshemu wanazopikia ni duni na mvua ikinyesha wanapata adha kubwa.

Kuwasaidia mikopo way majiko ya gas na mitungi yakewkwa riba nafuu kutaimarisha hata usafi wa mazingira wanayopikia, kuwaepusha na shida ya moto kuzimika mvua ikinyesha, kuokoa misitu yetu nk.

Serikali inaweza kufanya mkataba na makampuni ya gas ili kuwapa mama lishe uwezo wa kumiliki majiko bora.
 
Wanaweza kukopeshwa lakini je gesi itawalipa kuliko mkaa/kuni wanazotumia? Wasije wakashindwa kuendelea na gas wakarudi kule kule
 
Nadhan hii ni jambo zuri ila linaweza kufanya hata na kampuni binafsi kuwakopesha na kulipa kidogo kidogo...
Kwa mbaaali ni fursa nzuri sana kwa wauza mitungi na majiko ya gasi
 
Wanaweza kukopeshwa lakini je gesi itawalipa kuliko mkaa/kuni wanazotumia? Wasije wakashindwa kuendelea na gas wakarudi kule kule
Waangalie gharama na wanaweza kuipanua katika bei za vyakula vyao.
 
Waangalie gharama na wanaweza kuipanua katika bei za vyakula vyao.
Nadhani kwanza wao waseme kama wanaweza kutumia gas na ikawalipa. Kuna ambao wana mentality kuwa gas ni gharama ndio maana wanatumia kuni na si kama hawana uwezo wa kutumia gas
 
Back
Top Bottom