A
Anonymous
Guest
Serikali imeshindwa kulinda na kufuata Sheria na kanuni zake kama zinavyotaka...
Mfano, kuna Baraza la taifa la usimamizi na uhifadhi mazingira kazi yake kubwa kulinda na kusimamia Sheria ya mazingira ya mwaka 2004, ukisoma zaidi vifungu vyake vya 39 utagundua hazitekelezwi.
Kila kata na vijiji (hadi vitongoji) vinapaswa kuwa na mtaalam wa mazingira (Afisa Mazingira) lakini kwa nchi yetu hicho hakipo. Badala watumie kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kuanzia hizi ngazi za chini na pia kuondoka au kupungiza changamoto ya uhaba wa ajira kwa vijana.
Kuna wasomi wengine hasa kwenye kada hii ya mazingira lakini serikali imekuwa kama haioni umuhimu wake na badala yake tumekuwa tukiimba utunzaji wa mazingira, kupanda miti tu - tukidhani mazingira ndo kupanda tu miti kumbe kuna namna nyingine mbali na hilo.
Mfano kudhibiti utupaji ovyo taka ngumu na taka maji kutoka majumbani na masokoni. Mwisho wa siku tunawaachia watendaji wa Kijiji na Kata ndo wanalisimamia hilo bila kuwa na utaalamu wake.
Je, ni lini serikali itaona mazingira na jambo mtambuka na sekta inayojitegemea yenyewe? Na pia kuwaweka hawa watu wa mazingira itasaidia kwenye ukusanyaji wa mapato ngazi za chini zitokanazo na vyanzo mbalimbali vya kimazingira.
Naomba iwasilishwe ili Serikali Ione namna kulitatua hili.
Ahsantee