Serikali iwavutie vijana graduates katika kilimo kwa kuwakopesha mashine za irrigation katika makundi. Hii itasaidia kuwaondoa mitaani

Serikali iwavutie vijana graduates katika kilimo kwa kuwakopesha mashine za irrigation katika makundi. Hii itasaidia kuwaondoa mitaani

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Dkt. Gwajima D

Bado kilimo kinaonekana kama kamali machoni mwa vijana wa mjini

Bado kilimo kinaoekana primitive katika fikra za vijana wa mjini.

Lakini naamini kilimo hichi ndio mkombozi wao wa kukosa ajira. Bado tuna ardhi kubwa sana nyingine za wanachi na nyingine za serikali zilizo tengwa kusubiria investors.

Graduates wanaotoka mahala flani wakusanyike hata kumi, huku wao wakipewa plan ya marejesho hata ya 5-10yrs or which ever mtakavyoona then waingie mashambani wafanye kilimo ambacho hawatategemea tena mvua.

Mashine hizi watakuwa wakipokezana wao kwa wao. Mashine hizo wapewe kwa kuambatannisha na elimu kuhusu aina ya kilimo wanachoenda kukifanya.
 
Unajua kama ile mikopo ya halmashauri ya 10% waliyo toa serikali kwa vikundi vya vijana hawapewi, Badala yake zina nunuliwa pikipiki zile za samia ndio wana pewa vijana kama mkopo , Nazo still wanachukua uvccm ,Hili na ushahidi nalo.

Na je wajua kama Mradi wa BBT wa husein bashe na Wizara ya Kilimo ni upigaji wa wazi ambapo vijana waliopo kule wana tumika tu siku za kupiga picha na video lakini hamna chochote kinacho endelea wame telekezwa , wali haidiwa ekari 5 na wengine 10 kwa kila mmoja lakini hadi leo hawajapewa zile pesa walizo toa wadau na serikali unajua ziliko enda ?
CONCLUSION Hakuna project ya serikali itayo wahi kufanikiwa zaidi ya upigaji.
 
Tafuta hapa JF mada zinazoeleza mambo mengi kuvusha nchi au ukweli kama utaona wachangiaji.
We leta mada za ccm,mpira na ngono yani unaweza kupata viwer na comment zaidi ya youtube
 
Baada ya muda hizo mashine za irrigation utakuta zimenyofolewa , watu wameenda kuuza spare parts.
 
Unajua kama ile mikopo ya halmashauri ya 10% waliyo toa serikali kwa vikundi vya vijana hawapewi, Badala yake zina nunuliwa pikipiki zile za samia ndio wana pewa vijana kama mkopo , Nazo still wanachukua uvccm ,Hili na ushahidi nalo.

Na je wajua kama Mradi wa BBT wa husein bashe na Wizara ya Kilimo ni upigaji wa wazi ambapo vijana waliopo kule wana tumika tu siku za kupiga picha na video lakini hamna chochote kinacho endelea wame telekezwa , wali haidiwa ekari 5 na wengine 10 kwa kila mmoja lakini hadi leo hawajapewa zile pesa walizo toa wadau na serikali unajua ziliko enda ?
CONCLUSION Hakuna project ya serikali itayo wahi kufanikiwa zaidi ya upigaji.
Inasikitisha sanaaaa mkuu
 
Ukiniambia ni wapi tumefikia kimafanikio Ile mikopo ya 10% kwa vijana ya halmashauri , hoja Yako itakuwa ya msingi sana
 
Serikali yetu haijawahi kuwa na mpango mahususi kwaajili ya kizazi kijacho,kila kitu kinachofanyika nikwaajili ya sasa na ikitokea mradi utakuwa wa kunufaisha vijana inaonekana nikama wanafanya makosa ya kisiasa.
Fikiria ardhi tuliyonayo na ukubwa wake, maziwa na madini hatuwezi kuwa na mpango kabambe juu ya vijana na kuanzisha mashamba ya umwagiliaji, viwanda vya Kati kuchakata mazao ya kilomo,mistu,uvuvi na madini!? Serikali ikiwekeza kwa vijana kwa muda wa miaka 20 kujenga miundo mbinu ,utaalam na usimamizi wa dhati, itavuna na kurudisha fedha uwekezaji na miradi hiyo kuicha kwenye mikono ya vijana hao na kujenga ajira kwa vizazi vijavyo.Tungeliweza kujenga kwa haraka uchumi na kuachana na hizi kasumba za kulewesha vijana uchawa na kudhani kuwa maisha yaenda kwa kuwa chawa wa wanasiasa na matajiri wachache.
 
Serikali yetu haijawahi kuwa na mpango mahususi kwaajili ya kizazi kijacho,kila kitu kinachofanyika nikwaajili ya sasa na ikitokea mradi utakuwa wa kunufaisha vijana inaonekana nikama wanafanya makosa ya kisiasa.
Fikiria ardhi tuliyonayo na ukubwa wake, maziwa na madini hatuwezi kuwa na mpango kabambe juu ya vijana na kuanzisha viwanda vya Kati kuchakata mazao ya kilomo,mistu,uvuvi na madini!? Serikali ikiwekeza kwa vijana kwa muda wa miaka 20 kujenga miundo mbinu ,utaalam na usimamizi wa dhati, itavuna na kurudisha fedha uwekezaji na miradi hiyo kuicha kwenye mikono ya vijana hao na kujenga ajira kwa vizazi vijavo.Tungeliweza kujunga kwa haraka uchumi na kuachana na hizi kasumbs za kulwesha vijana uchawa na kudhani kuwa maisha yaenda kwa kuwa Chama wa wanasiasa na matajiri wachache.
Duh Too bad
 
Back
Top Bottom