Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Mimi si mpenzi wa Yanga au Simba, su timu yoyote nchini au nje ya nchi.
Ila ilipofika jana jioni, usiku nikakutana na shabiki mmoja akilalamikia vikali kuahirishwa kwa mechi ya Yanga na Simba, iliyokuwa ifanyike jana mchana..
Nimefuatilia kiini cha tatizo.
Kimsingi tatizo ni watu wazima na akili zao kujitwwka ushirikina kichwani, huku wakijua watanzania tulio wengi ni waumini wa dini zetu iwe Ukristo au Uislamu.
Ushirikina upo, lakini kuuenzi katika shughuli za umma huo ni ushenzi na kutostaarabika.
Kwahili sakata la jana Serikali kupitia Wizara husika ikemee ushenzi huu unaoonyesha kuna watu ustaarabu kwao bado kabisa.