Serikali iwe makini, Urusi imekuja na mbinu hizi kuchukua vijana wa Kitanzania kwenda kupigana Ukraine

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Siku za karibuni nimekuwa nikiona matangazo mengine matandaoni ya kuwavutia vijana kwenda kusoma bure Urusi.

Kabla ya vita hii inayoendelea sikuwahi kuona matangazo kama haya

Sasa ukitazama kuna vijana kadhaa kutoka Afrika waliokuwa wanasoma huko wamefia vitani halafu wote walikuwa jela

Hii inaleta wasiwasi mkubwa, bahati nzuri watu wengi wamestuka ila wapo wajinga wachache wanaoweza kuingia mtegoni, serikali iwe makini

Screenshot_20230130-204401.png
Screenshot_20230129-185225.png
Screenshot_20230130-204740.png
Screenshot_20230130-204759.png
Screenshot_20230130-204501.png
 
Labda kama wewe siyo mfatiliaji, hizi scholarship zipo sna kabla hata ya vita. Me nimewahi kuapply 2019
Najua zipo kitambo, ila zilikuwa hazitangazwi kwa fujo hivi

Nchi kibao zinatoa scholarships, Uturuki, Morocco, UK, nk lakini huoni zilitangazwa kwa fujo hivi, nakutana na matangazo mawili kila siku
 
Siku za karibuni nimekuwa nikiona matangazo mengine matandaoni ya kuwavutia vijana kwenda kusoma bure Urusi.

Kabla ya vita hii inayoendelea sikuwahi kuona matangazo kama haya

Sasa ukitazama kuna vijana kadhaa kutoka Afrika waliokuwa wanasoma huko wamefia vitani halafu wote walikuwa jela

Hii inaleta wasiwasi mkubwa, bahati nzuri watu wengi wamestuka ila wapo wajinga wachache wanaoweza kuingia mtegoni, serikali iwe makini

View attachment 2500583View attachment 2500584View attachment 2500585View attachment 2500587View attachment 2500592
Hapo ubaya uko wapi? Wewe hujui maisha naona, watu wengi hapa Africa wanatamani kujiuga na jeshi la Urusi ukipewa hiyo Fursa, mbona ni bonge la dili, kifia uko ni bahati mbaya tu.
 
Ngoja warusi was buza watuletee mwongozo
 
Najua zipo kitambo, ila zilikuwa hazitangazwi kwa fujo hivi

Nchi kibao zinatoa scholarships, Uturuki, Morocco, UK, nk lakini huoni zilitangazwa kwa fujo hivi, nakutana na matangazo mawili kila siku
Kongole mkuu. Kwa kweli ni kuchukua Tahadhari na kwa bahati nzuri Tz tunao uzoefu wa hili. Nchi ikiwa kwenye vita karibu mambo yote hudorora au kusitishwa kabisa kwani fedha nyingi hutumika vitani. ref.wakati Tz ipo vitani i.e.Tz vs Uganda(Iddi Amin) . Sasa tujiulize, hivi inakuwaje huyu mwamba yupo kwenye mapambano/vita kali halafu anatoa offer za scholarship nje-njee? Sio kwamba mwamba anajua watakaohitaji hizo "nafasi" ni vijana. Na vijana ndo wanatakiwa vitani. Watajileta wenyewe kwa hii chambo.
 
Apply na Sasa au mwambie mdogo wako afanye application
Nimeshaomba, sijawahi kuacha fursa. 2019 sikua tu na passport. Niliapply, sehemu ya passport ilikuwa lazima me nikaweka copy ya nida na namba. Passport imepatikana tayari deadline ilikuwa imepita.

Kuna mwana wa mtaa yupo kule anamalizia mwaka huu masters. Sasa unaogopa kwenda russia, unawez jaribu harakati alizopitia Justine Marack wakati anaenda kutafuta madini congo?

Kwani wewe ni ke au me? Nisije nikawa nakomaa na wewe kumbe mwanamke. Kama ni mwanamke sawa, upo sahihi kuogopa lakini kama ni mwanaume unazingua sana.
 
Hapo ubaya uko wapi? Wewe hujui maisha naona, watu wengi hapa Africa wanatamani kujiuga na jeshi la Urusi ukipewa hiyo Fursa, mbona ni bonge la dili, kifia uko ni bahati mbaya tu.
Mkuu mimi nimeshawatumia meseji whatsapp waniunge na hilo jeshi hata leo. Kufa kupo tu. Nashangaa sana mwanaume kushupaza shingo eti anaogopa kifo. Usipoenda russia/vitani ndio hutakufa? Mleta mada ni mgeni sana.
 
Najua zipo kitambo, ila zilikuwa hazitangazwi kwa fujo hivi

Nchi kibao zinatoa scholarships, Uturuki, Morocco, UK, nk lakini huoni zilitangazwa kwa fujo hivi, nakutana na matangazo mawili kila siku
Hivi Morocco unaenda kusoma Nini?
 
Nimeshaomba, sijawahi kuacha fursa. 2019 sikua tu na passport. Niliapply, sehemu ya passport ilikuwa lazima me nikaweka copy ya nida na namba. Passport imepatikana tayari deadline ilikuwa imepita.

Kuna mwana wa mtaa yupo kule anamalizia mwaka huu masters. Sasa unaogopa kwenda russia, unawez jaribu harakati alizopitia Justine Marack wakati anaenda kutafuta madini congo?

Kwani wewe ni ke au me? Nisije nikawa nakomaa na wewe kumbe mwanamke. Kama ni mwanamke sawa, upo sahihi kuogopa lakini kama ni mwanaume unazingua sana.
Sawa ukifika usisahau kutupa mrejesho
 
Back
Top Bottom