Jabali Jiwwe
Member
- Jul 28, 2022
- 7
- 8
Leo nipo ndani ya jukwaa letu, jamii forums nataka kuchangia mawazo naamini mamlaka yetu hasa serikali na wadau wote inaweza kutibu kabisa baadhi ya changamoto kubwa hasa katika mfumo mzima wa sekta ya kilimo.
Nina machache sana lakini naona ni ya msingi sana hasa yakitatuliwa hasa changamoto na kuboresha panapostahili.
Katika sekta yetu leo nitakuwa na hoja nne hasa nikieleza changamoto na nini kifanyike kwa wadau na serikali yetu hasa kuweza kuimarisha sekta hii muhimu kwa nchi yetu
Mosi, tumekuwa na sera kadhaa zinazogusa moja kwa moja katika sekta yetu yenye mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi hii ya kilimo. Nizungumzie hasa elimu ya kilimo katika shule zetu kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu
Changamoto hasa ipo katika utoaji wa elimu ya somo la kilimo, sote tunajua elimu ya kilimo haitolewi kabisa elimu ya msingi na kwa sekondari bado ni somo la hiari (jaribu kuwaza hapa) kwa elimu ya kidato cha tano na sita bado kwa nchi nzima tuna shule 16 pekee zinazoweza kuzalisha vijana watakaoenda elimu ya kati na juu ili kupata wataalamu katika sekta hii.
Muda huo pia unakuta shule hizo zina waalimu wachache sana. Bado kuna eneo hili somo hili kwa kiwango cha chuo cha kati na juu, waalimu wa masomo haya wanekuwa wakichukuliwa hata wenye mchepuo wa PCB na CBG kusoma BSC with science(agriculture na biology) kwa chuo kikuu sokoine, hii haitoi kile kilicho kusudiwa kwa vijana, ni sawa na mtu aliyesoma HISTORI na GEOGRAFIA na ENGLISH aende chuo kikuu kubobea somo la kiswahili
Pili, nitazungumzia wataalamu wetu hasa ma bwana shamba (extension officer)
Juzi tumeona wakikabidhiwa pikipiki pale Dodoma, kwa maoni yangu, serikali inalo jambo la kufanya zaidi ya kilichopo sasa, kwanza idadi yao ni ndogo kulinganisha na idadi ya wananchi wanaohitaji huduma yao
Nimepitia tafiti kadhaa zikieleza kuwa wakulima 25000 wanahudumiwa na bwana shamba mmoja!
Huu uwiano hauendani hasa kwenye kutoa huduma bora zinazolenga kuleta tija katika kilimo chetu.
Naishauri serikali na wadau hasa sekta binafsi ziwekeze katika eneo hili kwa nguvu na kwa kutenga bajeti nzuri itakayo kidhi mahitaji ili wakulima wanufaike na tuzidi kuongeza tija na mchango wa kilimo kwa uchumi wetu
Tatu, nimependa hatua zinazoanza kuchukuliwa na serikali hasa kwenye kuimarisha miradi ya kilimo cha umwagiliaji, wazo hili nadhani serikali ilivalie nzuga, hasa maeneo ya vijijini waweke miundombinu za umwagiliaji,
Sekta hii inaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na wakulima watakuwa wanufaika wakubwa hasa maeneo ya vijijini
Kwa kuanzia serikali itenge eneo moja au mawili kwa kila kanda ya kuanzisha miradi ya umwagiliaji, hasa kwa kuzingatia kila kanda (zones) inazalisha mazao gani na yananufaisha vipi wananchi na nchi kwa ujumla! Hii inaweza kufanyika mfano kanda ya ziwe kuwe na mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha zao la pamba, na serkali nayo iwe na mradi wa kiserikali utakaotumika kama darasa kwa wakulima (plantation)
Hii itakuwa kwa kanda zote za nchi kwa kuangalia kazao yanayostawi zaidi maeneo husika
Nne, kuimarisha masoko kwa wakulima, masoko kwa sasa ni tatizo sana kwa wakulima, serikali iamue kwa makisudi kuboresha masoko ya mazao yote, hii itaanzia kwenye huduma mhimu wakati wa uzalishaji wa mazao
Mfano mzuri kwenye mikopo ya subsidies(pbejeo za kilomo)
Hapa nimeona baadhi ya wahusika wakifanya urasimu, kwa macho yangu niliona mwaka 2018 kijiji kimoja kilichopo wilaya ya Igunga, wataalamu wa kilimo ikiwemo bwana shamba wa wilaya na kata waliamua kuwaza wakulima baada ya kuwakopesha dawa ya kuulia wadudu waharibifu wa pamba
Walichokifanya walileta dawa za kuua wadudu wanaobungua mahindi waliamua kubandika lebo za kuonesha ni wadudu wakulao pamba kumbe sivyo
Baada ya uchunguzi wa mmoja wanmkulima kubanduail ile lebo alikutana lebo nyingine ya hilo kopo ikiwa linaonesha ni dawa ya kuua wadudu wabungua mahindi
Kitu kama hichi ni kibaya mno kinarudisha nyuma jitihada za wakulima katika uzalishaji
Nadhani kama nchi ione kilimo ni sekta nyeti, iwe na mipango, sera na bajeti nzuri ya kufanya yote ya kuendeleza hii sekta kwa manufaa ya nchi yetu
Binafsi sioni mopango endelevu na yenye tija kuanzia shuleni hasa msingi hadi elimu ya juu, waweke sera kuanzia chini yenye maono ya mbali kuinua kilimo.

Upvote
1