Serikali iweke mpango wa kuangamiza kunguru, wanaharibu mazao na kusababisha hasara kubwa

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
Chonde chonde Serikali yetu, wakulima sasa tunapata shida kubwa hasa maeneo yetu huku Pwani

Mazao karibu yote yanasakamwa na kunguru, wanaharibu mazao kama, Tikiti maji, sweatmelon, sweatcon, mahindi ya kawaida,

Imeniuma sana nimelima hekari mbili ya Tikiti maji, yote yameharibiwa kwa kudonolewa yakiwa machanga

Kunguru saa 11 alfajiri tayati wapo shamba,

Tuna sikia kunguru hawa waliletwa kwa kazi maalumu ya usafi huko beach, basi serikali ione namna ya kuwaangamiza na au kuwapunguza kabisa

Kunguru wanavamia mpaka mboga, ugali na mchele wanakula

Kunguru wanasababisha umasikini
 
Hawa kunguru tolea jipya sasa hivi wanaamka saa 9 usiku wanaamshana.

Ni janga la Taifa, hawafai kabisa si kwa wakulima tu hata mjini ni kero kubwa sana.
 
Tafuta vijana walipe wawauwe kama ishirini, uwatupe sehem tofauti kwenye hilo eneo, wakimaliza msiba watahama wote
 
Wawauwe kwa kutumia nini?, hawa kunguru wajanja mno...Atengeneze mtego wa nondo zinasukwa vizuri, inaachwa sehemu ya juu ya kuongia ndani lkn hawezi kutoka kupitia hapo. Huo mtego unajengwa kama kibanda hivi ,humo ndani panawekwa mabaki ya chakula...wiki tu wote wameisha.
 
Tafuta vijana walipe wawauwe kama ishirini, uwatupe sehem tofauti kwenye hilo eneo, wakimaliza msiba watahama wote
Nina mizoga minne boss, mwanzoni wakiona wanaogopa, baada ya siku kadhaa wanaendelea na uharibifu
 
Back
Top Bottom