UTANGULIZI
Ni ukweli usiopingika kwamba, Watanzania wengi wamebarikiwa kuwa na vipaji mbalimbali. Mfano, Utengenezaji wa bidhaa, ubunifu wa vyombo vya kielektroniki, uchoraji, uchongaji, matumizi ya compyuta, uimbaji nk.
Licha ya Tanzania kuwa na vijana wengi wenye vipaji, bado kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kutafuta kuajiliwa badala ya kutumia vipaji vyao katika kujiajili.
Vijana wengi wana malengo ya kujiajili kupitia vipaji vyao, lakini kutokana na changamoto mbalimbali katika mifumo ya sera za kitaifa, wadau wa uchumi na biashara, pamoja na jamii kwa ujumla, zimesababisha vijana hao kukosa msaada wa kutumia vipaji vyao kama mitaji ya kujiajili.
Katika Makala hii tutaangalia hatua mbalimbali ambazo Serikali, Wadau wa masuala ya uchumi na jamii kwa ujumla wanaweza kuchukua ili kuleta mapinduzi ya vipaji vya watanzania katika kukuza uchumi kwa wenye vipaji na taifa kwa ujumla.
Nchi nyingi duniani zimekuwa na viwanda vikubwa na matajiri wakubwa kutokana na kutoa sapoti kwa vijana wenye vipaji. Mfano, Elon Musk, mwanzilishi wa kampuni ya utengenezaji magari yanayotumia umeme – Tesla, amefanikiwa kuwa tajiri mkubwa sana duniani kutokana na ubunifu wake uliotokana na kipaji chake. Serikali yake imekuwa ikimpa ushirikiano mkubwa sana uliopelekea mafanikio yake. Mfano, serikali yake ya Marekani imetoa takribani dola billioni 4.9 ili kuwezesha kampuni yake kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Chanzo Times(Elon Musk's growing empire is fueled by $4.9 billion in government subsidies).
Serikali kupitia idara mbalimbali katika Halmashauri za wilaya, inaweza kutoa nafasi kwa Watanzania kuonyesha vipaji vyao na kuviratibu. Baada ya hapo upembuzi ufanyike ili kubaini vipaji ambavyo vinaweza kupewa sapoti na vipaumbele ili kukuzwa kuwa viwanda vidogo vidogo.
Hali hii itapelekea vijana wengi kupata ajira, na uzalishaji wa bidhaa za kitanzania utaongezeka badala ya kutegemea ununuzi wa bidhaa zinazotengenezwa na vijana wenye vipaji kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.
Ikiwa serikali itafanikiwa katika hili, tutaona mabadiliko makubwa sana katika mapinduzi ya viwanda na hatimaye uchumi wetu wa Tanzania utakua kwa kasi kubwa.
Baadhi ya vipaji vya watanzania vinahusiana na utoaji huduma kwa njia ya kimtandao, yaani kupitia tovuti au program tumishi (Apps). Mfano, vipaji kama uchoraji, utengenezaji wa program za kompyuta, uigizaji, uimbaji nk, hufanikiwa Zaidi pale kazi zake zinapouzwa kupitia njia za kimtandao, kwasababu njia hii ina uwanja mpana wa soko (ndani na nje) ya mipaka ya nchi. Changamoto kubwa katika nchi yetu ya Tanzania ni namna ya kupokea malipo kwa njia ya mtandao, yaani kupitia tovuti na program tumishi. Mfano, kupitia PayPal, wajasiriamali kutoka nchi mbalimbali wamefanikiwa sana kukuza biashara zao, kwani wanaweza kupokea malipo ya huduma au bidhaa zao kwa njia ya mtandao.
Hapa nchini Tanzania, mtu anaweza kutuma fedha kwenda nchi mbalimbali lakini hawezi kupokea fedha kupitia PayPal au huduma nyingine zinazowezesha biashara kupokea malipo kwa njia ya mtandao. Hii inaonekana ni kutokana na uwepo wa sharia na kanuni za kibenki ambazo haziendani sana na sharia za kibenki za kimataifa katika kutuma na kupokea fedha kwa njia ya mtandao.
Ikiwa serikali italiangalia hili, vijana wengi wenye vipaji ambavyo vinaweza kugeuzwa kuwa biashara, wanaweza kuuza bidhaa au huduma zao kwa njia ya mitandao kupitia tovuti ndani na hata nje ya nchi na hatimaye kuwepo kwa makampuni mengi yatakayokuza uchumi wa taifa.
HITIMISHO
Taifa linaweza kupata mapinduzi makubwa sana ya kiuchumi ikiwa wenye vipaji wataangaliwa kwa jicho la kibiashara. Nchi za wenzetu zimefanikiwa kwa hatua kubwa sana kugeuza vipaji kuwa fursa za kibiashara. Hii inatokana na namna serikali zinavyotoa misaada kwa wenye vipaji. Makampuni mengi yameanzishwa kupitia vijapi ambavyo mwanzo vilionekana ni ujinga, lakini leo hii ni vyanzo vikubwa vya mapato katika nchi za wenzetu.
Ikiwa Serikali, wadau wa masuala ya uchumi na jamii itawekeza kwenye vipaji, na mifumo ya malipo kwa njia ya mitandao, viwanda vingi, makampuni mengi yataanzishwa hali itakayochochea ukuaji wa uchumi wa Taifa letu - Tanzania.
WITO
Tuheshimu, tupende na kuwekeza Zaidi katika vile tulivyonavyo ndani ya nchi kuliko kutegemea sana vya nje ambavyo vinaweza kudhoofisha uwezo wa watanzania kufikiri katika kutengeneza bidhaa au huduma za ndani.

- Serikali iwekeze kwenye vipaji vinavyoendana na uzalishaji mali, kwa kuweka mpango wa kuratibu vipaji katika ngazi za wilaya ili kubaini vipaji vinavyoweza kukuzwa kuwa viwanda vidogo vidogo.
Nchi nyingi duniani zimekuwa na viwanda vikubwa na matajiri wakubwa kutokana na kutoa sapoti kwa vijana wenye vipaji. Mfano, Elon Musk, mwanzilishi wa kampuni ya utengenezaji magari yanayotumia umeme – Tesla, amefanikiwa kuwa tajiri mkubwa sana duniani kutokana na ubunifu wake uliotokana na kipaji chake. Serikali yake imekuwa ikimpa ushirikiano mkubwa sana uliopelekea mafanikio yake. Mfano, serikali yake ya Marekani imetoa takribani dola billioni 4.9 ili kuwezesha kampuni yake kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Chanzo Times(Elon Musk's growing empire is fueled by $4.9 billion in government subsidies).
Serikali kupitia idara mbalimbali katika Halmashauri za wilaya, inaweza kutoa nafasi kwa Watanzania kuonyesha vipaji vyao na kuviratibu. Baada ya hapo upembuzi ufanyike ili kubaini vipaji ambavyo vinaweza kupewa sapoti na vipaumbele ili kukuzwa kuwa viwanda vidogo vidogo.
Hali hii itapelekea vijana wengi kupata ajira, na uzalishaji wa bidhaa za kitanzania utaongezeka badala ya kutegemea ununuzi wa bidhaa zinazotengenezwa na vijana wenye vipaji kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.
Ikiwa serikali itafanikiwa katika hili, tutaona mabadiliko makubwa sana katika mapinduzi ya viwanda na hatimaye uchumi wetu wa Tanzania utakua kwa kasi kubwa.
- Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania iweke mifumo mizuri ya kibenki, itakayowezesha watu kufanya biashara za kimitandao (Online Business) na kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia ulimwenguni.
Baadhi ya vipaji vya watanzania vinahusiana na utoaji huduma kwa njia ya kimtandao, yaani kupitia tovuti au program tumishi (Apps). Mfano, vipaji kama uchoraji, utengenezaji wa program za kompyuta, uigizaji, uimbaji nk, hufanikiwa Zaidi pale kazi zake zinapouzwa kupitia njia za kimtandao, kwasababu njia hii ina uwanja mpana wa soko (ndani na nje) ya mipaka ya nchi. Changamoto kubwa katika nchi yetu ya Tanzania ni namna ya kupokea malipo kwa njia ya mtandao, yaani kupitia tovuti na program tumishi. Mfano, kupitia PayPal, wajasiriamali kutoka nchi mbalimbali wamefanikiwa sana kukuza biashara zao, kwani wanaweza kupokea malipo ya huduma au bidhaa zao kwa njia ya mtandao.
Hapa nchini Tanzania, mtu anaweza kutuma fedha kwenda nchi mbalimbali lakini hawezi kupokea fedha kupitia PayPal au huduma nyingine zinazowezesha biashara kupokea malipo kwa njia ya mtandao. Hii inaonekana ni kutokana na uwepo wa sharia na kanuni za kibenki ambazo haziendani sana na sharia za kibenki za kimataifa katika kutuma na kupokea fedha kwa njia ya mtandao.
Ikiwa serikali italiangalia hili, vijana wengi wenye vipaji ambavyo vinaweza kugeuzwa kuwa biashara, wanaweza kuuza bidhaa au huduma zao kwa njia ya mitandao kupitia tovuti ndani na hata nje ya nchi na hatimaye kuwepo kwa makampuni mengi yatakayokuza uchumi wa taifa.
- Serikali ianzishe na kuwekeza katika siku ya vipaji Tanzania kama ilivyo nane nane na sabasaba.
- Jamii na wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi waache kukatisha tamaa walio na vipaji na badala yake watoe ushirikiano ili kukuza vipaji hivyo.

Upvote
10