SoC04 Serikali iwekeze zaidi katika Sekta ya Nishati

SoC04 Serikali iwekeze zaidi katika Sekta ya Nishati

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
30
Reaction score
12
Tanzania tuitatayo katika suala zima la nishati yafuatayo yakizingatiwa nadhani tutakuwa tumejenga na siyo kubomoa.

1. Kuhakikisha umeme unafika maeneo yote ambayo bado yako gizani na sio kusema umeme umezidi kiwango wakati maeneo mengine hata nguzo za umeme hawajui zinafananaje.

2. Bei ya kuunganishiwa umeme iwe kwenye kiwango ambacho hata mtanzania mwenye maisha duni anaweza kumudu na sio kama ilivyo kwa sasa.

3. Kuhakikisha bei ya gesi inafkia kiwango kizuri ili mtanzania yeyote aweze kutumia gesi. Sio kushauri watu waachane na matumizi ya mkaa watumie gesi na wakati gesi bei yake ipo juu.

4. Kuongeza uzalishaji wa vyanzo mbalimbali vya nishati ili kukabiliana na changamoto ya bei kwa baadhi ya bidhaa mfano petroli na gesi.

Screenshot_20240501-122657.png

5. Kupanua wigo wa utendaji kazi katika sekta ya nishati ili kutengeneza nafasi za ajira kwa vijana waliopo mtaani hawana kazi na wakati wana taaluma zao

6. Kuongeza mbinu zenye kuweka uimara wa baadhi ya miundo mbinu inayohusika na nishati mfano nguzo za umeme waweke zenye uimara nasio hizi ambazo mara tunakuta zimeanguka mara zimeoza kwa chini.

7. Kutoa elimu mara kwa mara kwa watanzia kuhusiana na matumizi sahihi ya umeme, gesi na vyanzo vingine vya nishati ili kuepusha majanga kama mlipuko wa moto n.k.
 
Upvote 1
Umegusia kitu muhimu sana.

Nishati.

Nguvu ya watumwa wapatao mia nyumbani kwako......... Tunaitaka Tanzania yenye umeme wa kumwaga. Na uwezo tunao.
Asante.
 
Back
Top Bottom