Serikali kuacha kutumia nguzo za miti ili kuzuia ukatikaji wa umeme hasa sehemu zenye mafuriko

Serikali kuacha kutumia nguzo za miti ili kuzuia ukatikaji wa umeme hasa sehemu zenye mafuriko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Picha

SERIKALI itaachana na matumizi ya nguzo za umeme zitokanazo na miti na badala yake itatumia nguzo za zege ili kuepukana na uharibifu wa nguzo kuoza na kusababisha tatizo la ukatikaji wa umeme.

Hayo yamesemwa wilayani Rufiji mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati alipotembelea kuona nguzo za zege 250 kutumika baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kwenye wilaya hiyo kupitia miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwenye wilaya za Rufiji na Kibiti.

Mgalu amesema mradi wa kuweka nguzo za zege umeanza kwa baadhi ya maeneo na mradi wa Kibaha na kwenye Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere na huo ni mpango kwa nchi nzima.

“Tumeanza kutumia nguzo za zege kwa ajili ya kusambaza umeme kwa miradi mbalimbali ambapo sehemu nyingine ni Muhoro ambako palikumbwa na mafuriko na kusababisha umeme kukosekana kwa zaidi ya mwezi hivyo ili kumaliza tatizo la umeme kukatika ni kuwa na nguzo za zege,” amesema Mgalu.

Amesema kwa Wilaya ya Rufiji watabadilisha kipande cha Daraja la Mkapa hadi Muhoro sehemu yenye matatizo ya mafuriko na kusababisha tatizo la umeme kukatika lakin nguzo za zege itakuwa suluhisho.

“Ukatikaji wa umeme hutokana na nguzo hizi za miti kuoza na kuanguka au pale yanapotokea mafuriko umeme hukatika hivyo kwa kutumia nguzo za zege ni suluhisho la ukatikaji wa umeme,” amesema Mgalu.

Aidha, amesema sasa vijiji ambavyo havina umeme Pwani ni 89 ambavyo vimewekwa REA awamu ya tatu mzunguko wa pili ambao kwa sasa uko kwenye mchakato wa kutangaza tenda kwa wakandarasi.

“Kwenye awamu hii ya tatu mzunguko wa pili wa utekelezaji mradi huo utakuwa ni wa miezi 12 ambapo tutaboresha utoaji kandarasi kwa kutowarundikia kazi nyingi kama ilivyo sasa kwa wakandarasi kuwa na mkoa zaidi ya mmoja ambapo lengo ni kutaka wakamilishe kazi kwa wakati,” amesema Mgalu.

Amesema matarajio ni kuhakikisha mwakani vijiji vyote vina umeme, ambao Pwani miaka mitano iliyopita vijiji vilivyokuwa na umeme ni 79, lakini kwa sasa vijiji 342 vina umeme, Sh bilioni 138 zikitolewa. Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Ally Ungando alisema vijiji 41 vina umeme na vijiji 17 ndiyo vilivyobaki na hivyo viko kwenye Delta ambako wilaya hiyo ina vijiji 58.
 
Ni kweli .hiyo ni suluhisho ya kudumu.na kwa upande mwingine ni kifo kitakatifu kwa kampuni ya sao hill ambayo ilikuwa inatengeneza hizi nguzo
 
Hii ni alert kwa waliowekeza kwenye mistimu!
 
Naona posho za watu zinaeenda kufutwa na zitasaaidia sana kukatika umeme mara kwa mara hasa sehemu zenye maji maji.
 
Hii itasaidia watu wanaoishi msituni umeme unakatika sana wakati wa mvua kutokana na kuanguka nguzo

Pia utunzaji wa mazingira
 
Nchi kama Msumbiji nguzo za mti huwezi kuzikuta. Sijui Tanzania tulijisahau wapi?
 
Back
Top Bottom