The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Serikali imedhamiria kuboresha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuijenga upya, ili kuwezesha huduma zote kutolewa ndani ya jengo moja litakalokuwa na vitanda 1,757 kutoka 1,435 vya sasa ambapo mradi huo utagharimu USD .468 Mil (takribani TZS. 1.2 Trilioni), ambapo kati ya fedha hizo USD.364 Mil zitatoka Korea Kusini na Serikali ya Tanzania itachangia USD. 104 Mil.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Rachel Mhaville kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH wakati akitoa taarifa kwa umma juu ya mafanikio ya kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kwa sasa upembuzi yakinifu wa mradi huo umekamilika hivyo hatua mbalimbali za kusaini mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Korea zinaendelea vizuri.
Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Hospitali ya Taifa Muhimbili yenye kampasi mbili ni Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa na kubwa kuliko zote nchini ina vitanda 2,043 ambapo Upanga kuna vitanda 1,435 na Mloganzila vipo 608.Katika kampasi zote mbili wagonjwa 4,000 wanaonwa kwa siku.