Serikali kuchelewa kulipa wakandarasi TANROADS, RUWASA; Je Serikali haina hela?

Serikali kuchelewa kulipa wakandarasi TANROADS, RUWASA; Je Serikali haina hela?

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Toka Awamu ya Mama aingie madarakani kumekuwa na ucheleweshaji wa malipo ya wakandarasi wnaofanya kazi na serekali.

Mwezi wa 11 mwaka jana Waziri Bashungwa alifanya kikao na wakandarasi moja ya malalamiko aliyapata ilikuwa na ucheleweshaji wa fedha za wakandarasi tofauti na miaka ya nyuma pomoja na yote alitoa bla blaa zake pale siasa nyingi lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika

Nakumbuka Kipindi cha aliamua kusitisha kutangazwa kwa kazi za miradi ya Maji mpaka pale RUWASA ilipokaa sawa na alisema hataki kuona miradi inatangazwa kama fedha hakuna, Dodoma pekee ilisainiwa miradi zaidi ya kumi lakini Miradi yote ni kama imesimama, fedha hakuna.

Aweso amekuwa ni mtu wa Sound vibaya sana kelele nyingi lakini hakuna anachokifanya.

Sasa hakuna Mkandarasi anatamani kufanya kazi miradi ya maji inayofadhiliwa na serekali.

Jambo la kushangaza kabisa TANROADS nako hali ni Tete hakuna hela, jambo ambalo halijawahi kutokea huko nyuma, nimesikia kubwa mwezi wa 12 TANROADS hali ilikuwa mbaya mapka mishahara ilitoka TBA.

Nashauri serikali kama hela hakuna, hakuna haja ya kutangaza miradi.

Wakandarasi wanaweka fedha yao kwenye miradi tena kwa kukopa kwenye Mabenki na suppliers, unapowacheleweshea pesa zao unawaweka kwenye wakati mgumu sana.
 
Wanachelewesha Pesa alafu chelewesha Kazi uone balaa lake[emoji23][emoji23][emoji23]

Unasemwa mbele ya vyombo vya habari na wanao wanakuna pale ulivyo uvyata mkia kama mmbwa alie pigwa jiwe
 
Hali mbaya Serekali haina hela
 
Mimi niliisha achana na ukandarasi wa Serikali. Tangu mwanzo wa kuomba kazi mpaka hatua ya malipo ni RUSHWA tupu.
 
Back
Top Bottom