BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Sakata la mwekezaji wa shamba la kuku wa nyama na mayai mkoani Kilimanjaro, kuteketeza kwa moto vifaranga 50,000 vya kuku kwa madai ya kukosa soko, limechukua sura mpya, baada ya serikali kusema inakusudia kuchukua hatua dhidi ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Mifugo, Prof. Hezron Nonga, alinukuliwa na kituo kimoja cha televisheni nchini, akisema kilichofanywa na mwekezaji huyo ni kinyume cha Sheria ya Ustawi wa Wanyama ya Mwaka 2010.
“Vifaranga wanawekwa kwenye matanuru ya moto, vifaranga vinalia machozi lakini vinachomwa moto ili viungue. Hiyo ni kinyume cha Sheria ya Ustawi wa Wanyama ya Mwaka 2010. Serikali tunakusudia kuchukua hatua dhidi ya kampuni ile kwa kitendo ilichofanya,” alisema.
Desemba 13, mwaka huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anayesimamia sekta ya mifugo, Tixon nzunda, wakati anafungua kikao cha wadau wa tasnia ya kuku, kilichofanyika jijini Dodoma, alinukuliwa akiwataka wazalishaji wa vifaranga vya kuku nchini kuzalisha vifaranga kwa kuzingatia ubora wa kitaifa na kimataifa na mahitaji yaliyopo.
Kikao hicho kilikuwa kikijadili hali ya upatikanaji na bei ya vifaranga na vyakula vya kuku pamoja na kushuka kwa soko na bei ya kuku wa nyama nchini.
Kwa mujibu wa wavuti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, pia kikao hicho kilijadili namna ya kupunguza gharama za uzalishaji wa kuku, hasa wa nyama ikiwa msingi mmojawapo wa kuwawezesha wafugaji wadogo na walaji kumudu gharama.
Pia wadau hao walijadili kuhusu gharama kubwa za utengenezaji wa chakula cha kuku, ili kuona namna gani wanaweza kuzipunguza, na hivyo kumsaidia mfugaji kupunguza gharama za ufugaji.
Mkurugenzi huyo alipoulizwa kuhusu malalamiko ya utoaji wa vibali vya uingizaji wa vifaranga unaolalamikiwa na wengi, alisema: “Tumekuwa tukiwaeleza kwamba vifaranga hawa wanaoendelea kuruhusiwa, walikuwa wameshalipiwa kabla ya katazo.
“Kwa hiyo sasa, serikali haikuwa na sababu yeyote ya kuwakatalia hawa wakati walishalipia vifaranga, na ndio ambao tumeendelea kuwaruhusu kuingiza vifaranga, lakini ukomo wa kuingia kwa vifaranga hivi itakuwa ni Desemba 31, mwaka huu,” mwaka huu.
Kuhusu wafanyabiashara wachache ambao wamesalia kuingiza vifaranga, alisema wafugaji wengi hasa wa kuku na nyama wameacha kufuga.
“Aidha wamefunga kabisa mabanda au wamepunguza idadi ya kuku waliokuwa wanafuga. Kama mtu alikuwa anafuga kuku 2,000 kwa wakati mmoja utakuta anafuga kuku 200 kwa wakati mmoja.
“Kwa nini hao watu wameacha kufuga, moja, chakula cha kuku kimepanda bei sana. Kilikuwa kinauzwa 65,000 mpaka 70,000 kwa mfuko wa kilogramu 50, sasa hivi chakula cha kuku kinauzwa kwa shilingi 90 mpaka 95 kwa mfuko wa kilogramu 50,” alisema.
“Kuku 500 wanakula mfuko mmoja kwa siku, sasa huyu mfugaji akipiga hesabu pale hakuna atakachokipata. Ukiweka gharama za chakula, mambo ya maji, chanjo, madawa na huduma zingine, huyu mfugaji hakuna anachokipata sana sana anapata hasara.
“Pamoja na hao kuku anaowafuga kwa hasara, bado bei ya kuku imepungua sana. Zamani bei ya kuku Dar es Salaam, kuku mmoja wa nyama alikuwa anauzwa kwa Sh. 7,000 mpaka 8,000. Sasa hivi anauzwa Sh. 4,000 hadi 5,000,” aliongeza.
Alipoulizwa serikali inawasaidiaje wafugaji hao wa kuku, Prof. Nonga alisisitiza ni lazima wafugaji wajue kwamba kuna msimu wa mavuno sana na kuna msimu wa hasara.
“Walivuna sana kipindi mahitaji ya vifaranga ni makubwa, walikuwa wanauza mpaka 2,500 na bado mtu analipia leo vifaranga 5,000 anasubiri mpaka miezi mitatu. Hiki ni kipindi cha mpito, hali itatengemaa tu. Kufikia mwishoni mwa mwezi huu, vifaranga watapanda tu bei.” alisema.
Zaidi ya vifaranga 50,000 vya kuku wa nyama na mayai vimeteketezwa kwa moto mkoani Kilimanjaro kwa madai ya kukosa soko kutokana na kuwapo kuku wanaoingizwa kutoka nje ya nchi kuathiri soko la ndani.
Mwekezaji huyo wa shamba la kuku (jina limehifadhiwa), akizungumzia uamuzi wake wa kuvichoma moto vifaranga hivyo, alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu hali ya soko la kuku nchini kwa sasa si la kuridhisha kutokana na wafugaji kupata hasara baada ya wafugaji kutumia gharama kubwa za uzalishaji.
“Sasa tuna mayai 8,000 kwenye mashine, tunatotoa kila wiki 2,000 lakini hakuna biashara. Siku nne zilizopita tuliuza vifaranga kwa Sh. 1,000 mpaka 900 watu hawataki. Umeona mwenyewe vifaranga 34,000 vimerudi havina biashara,” alisema mwekezaji huyo.
Hivi karibuni, wafugaji waliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kudhibiti vifaranga kutoka nje,ambavyo vimejaa sokoni huku bei ya chakula ikizidi kupaa na kuwalazimu kuuza kwa bei ya hasara Sh. 4,000 kutoka 6,500.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Kuku wa Nyama Tanzania (TABROFA), Aloyce Makoye, alisema hali sio ya kuridhisha na watu wanalazimika kuachana na biashara hiyo, lakini serikali imeendelea kuruhusu vifaranga kutoka nchi mbalimbali.
NIPASHE