JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kutokana na kuwapo idadi kubwa ya madaktari vijiweni, Serikali imesema ipo katika mchakato wa ufumbuzi wa tatizo hilo, ikigusia kuwa itaanza kudhibiti wale wanaofanya kazi hospitali zaidi ya moja na vituo vya afya binafsi.
Zaidi ya madaktari 5,000 waliohitimu na kuwa na sifa za kuajiriwa, bado wanaendelea kusota mtaani kwa kukosa ajira rasmi, wanaokadiriwa kutumia zaidi ya Sh450 bilioni kusomea fani hiyo.
Hayo yamesemwa leo Jumanne, Julai 30, 2024 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu katika Kongamano la Kumbukizi ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, hayati Benjamini Mkapa linalofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri Ummy amesema madaktari wameruhusiwa kuanzisha hospitali zao baada ya muda wa kazi, lakini kinachoonekana sasa daktari mmoja anafanya kazi zaidi ya vituo viwili, hivyo kuminya ajira za madaktari wengine waliopo mtaani.
“Kama kwenye mpira wachezaji wa nje wasizidi kadhaa, inakuja na kwenye sekta ya afya kama una hospitali tutakupa maelekezo, asilimia kadhaa ya unaowaajiri wasiwe kwenye ajira za kudumu, mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sasa tunafanya uchambuzi tutakuja kwako baada ya kuwa tumemaliza huu uchambuzi,” amesema Waziri Ummy akimfahamisha Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
Chanzo: Mwananchi