Serikali Kuendelea Kuhamasisha Uwekezaji na Uendelezaji wa Viwanda Nchini - Mhe. Kigahe.

Serikali Kuendelea Kuhamasisha Uwekezaji na Uendelezaji wa Viwanda Nchini - Mhe. Kigahe.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Serikali kuendelea kuhamasisha uwekezaji na uendelezaji wa viwanda Nchini-Mhe.Kigahe.

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe amesema kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vipya na uendelezaji wa viwanda vilivyopo katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi hususani Viwanda vya kuchakata mazao ya Mifugo na Uvuvi vikiwemo viwanda vya Nyama na Samaki katika Mkoa wa Rukwa na mikoa mingine nchini.

Mhe.Kigahe amebainisha hayo Septemba 8,2023 Bungeni Jijini Dodoma alipojibu swali la Mhe.Bupe Nelson Mwakang'ata linalotaka kufahamu kuwa ni lini Serikali itaviendeleza viwanda vya nyama na samaki mkoani Rukwa.

Aidha Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka nguvu kubwa katika unenepeshaji wa mifugo pamoja na ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba, kutenga na kuboresha maeneo ya kukusanyia samaki (collection Centers) pamoja na minada ya mifugo ili kukidhi haja ya upatikanaji endelevu wa malighafi bora ya viwanda vya nyama na samaki nchini.

Vilevile Mhe.Kigahe ametoa rai kwa wavuvi na wafugaji kuviuzia malighafi viwanda vya ndani ili viweze kukidhi mahitaji yake.​

 

Attachments

  • F5izZGxXUAA6YCE.jpg
    F5izZGxXUAA6YCE.jpg
    125.6 KB · Views: 3
  • F5izZecXYAAJpyW.jpg
    F5izZecXYAAJpyW.jpg
    125.2 KB · Views: 3
  • F5izZ3WWUAAG5QD.jpg
    F5izZ3WWUAAG5QD.jpg
    122.2 KB · Views: 3
  • F5izaRgXMAALj3c.jpg
    F5izaRgXMAALj3c.jpg
    116.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom