Serikali Kufufua Kilimo cha Umwagiliaji Kwenye Bonde la Bugwema

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

AHADI YA MHESHIMIWA RAIS YATEKELEZWA - SERIKALI KUFUFUA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KWENYE BONDE LA BUGWEMA​

Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipokea na kukubali ombi la kufufua kilimo cha Umwagiliaji kwenye Bonde la Bugwema la Musoma Vijijini.

Ombi hilo la Wana-Musoma Vijijini liliwasilishwa kwa Mhe Rais na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo. Hii ilikuwa tarehe 6.2.2022, siku ambayo Mhe Rais aliweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama (thamani: Tsh bilioni 70.5)

Serikali iliyoongozwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilianza kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwenye Bonde hilo Mwaka 1974. Mradi ukasimama, na sasa unafufuliwa!

Ukubwa wa Bonde la Bugwema:
Bonde hili ni kubwa mno ambapo vijiji vyote vitatu kwa Kata ya Bugwema vimo ndani yake. Vijiji hivyo ni Bugwema, Masinono na Muhoji. Hili eneo pekee lina ukubwa wa zaidi ya Hekta 6,000 (elfu sita).

Baadhi ya maeneo ya Kata jirani za Bugoji, Nyambono na Murangi ni sehemu ya Bonde hili kwa upana na urefu wake, ambapo kwa ujumla wake Bonde linakadiriwa kuwa na ukubwa wa zaidi ya Hekta 10,000 (elfu kumi)

Mazao yanayolimwa ndani ya Bonde la Bugwema:
*Mpunga, mahindi, alizeti, dengu na pamba ndiyo mazao makuu yanayolimwa ndani ya bonde hili.

Bajeti 2023/2024 - Tume ya Taifa ya Umwagiliaji:
Tume hii imetoa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu (feasibility study & design) wa Bonde la Bugwema kwa Kampuni ya Ms MHANDISI CONSULTANCY LTD. Kazi zinaanza mwezi huu (August 2023).

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa - Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akiwa na baadhi ya wakulima na wafugaji wa Bonde la Bugwema, Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumapili, 20.8.2023
 
Attachments

  • WhatsApp Video 2023-08-20 at 16.54.48.mp4
    21.5 MB

Naweza kupata shamba huko?
 
Back
Top Bottom