Serikali Kufufua Kiwanda cha Nguo cha MUTEX Musoma

Serikali Kufufua Kiwanda cha Nguo cha MUTEX Musoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
GHATI CHOMETE - SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA NGUO MUTEX MUSOMA

MASWALI NA MAJIBU BUNGENI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe. Ghati Zephania Chomete ameiuliza swali Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambalo lilijibiwa na Naibu Waziri Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe

"Pamoja na Uwekezaji mzuri kufanyika wa kujenga kiwanda cha nguo cha MUTEX Musoma , lakini mpaka sasa kiwanda hakifanyi kazi, Ni upi mkakati wa Serikali wa kufufua kiwanda hicho"? - Mhe. Chomete

"Moja ya mikakati ya Serikali ni kuona namna gani tunafufua Viwanda ambavyo havifanyi kazi. Serikali tumeshaanza kuona vile Viwanda ambavyo walikuwa wamepewa watu binafsi na havifanyi kazi na hawaviendelezi kuvirudisha Serikalini na hatua ya pili ni kuvitafutia wawekezaji ili waweze kuwekeza katika Viwanda hivyo na mojawapo ni kiwanda cha MUTEX Musoma" - . Exaud Silaoneka Kigahe

Watatumia teknolojia ya kisasa ambayo inapunguza gharama ya uzalishaji au ni mwendo wa ukarabati wa mitambo awamu ya kwanza ambayo ilifaa tu kushona kaniki!?
 
Watatumia teknolojia ya kisasa ambayo inapunguza gharama ya uzalishaji au ni mwendo wa ukarabati wa mitambo awamu ya kwanza ambayo ilifaa tu kushona kaniki!?
[emoji38] [emoji23] [emoji38]
Mbona kaniki
Kama kawaida ni mwendo wa spana mkononi

Technology mpya bado sana kwa wapigaji
Kuna machine za hospitali bado hazijafunguliwa wilayani hawajui namna ya kuzitumia
 
Watatumia teknolojia ya kisasa ambayo inapunguza gharama ya uzalishaji au ni mwendo wa ukarabati wa mitambo awamu ya kwanza ambayo ilifaa tu kushona kaniki!?
Hiv viwanda vingi kwa sasa yamebaki majengo tu, ukitaka kuwekeza inabidi utoe mitambo yote uweke mipyaaaa

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom