Mangi Mkubwa
Senior Member
- Jan 3, 2014
- 107
- 29
SERIKALI KUFUTA USHIRIKA WA G32 NI NJIA SAHIHI YA KUFUFUA USHIRIKA WA KNCU MKOANI KILIMANJARO?
Wakuu hongereni na majukumu ya kila siku naomba niwaletee yanayojiri Mkoani kwangu kuhusu masuala ya Ushirika ambao ilikuwa na mchango mkubwa sana wa kiuchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Hivi karibuni Serikali imetangaza kufuta ushirika wa vyama 32 na kuagiza shughuli zake pamoja na vyama hivyo vya msingi kuhamia chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro KNCU.
Uamuzi huu umefanywa na mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Dk Benson Ndege ambapo kwa maelezo yake ni kwamba anafuta ushirika huo wa G32 kwa kuwa unafanya kazi inayofanana na ile ya KNCU.
Katika barua yake ya anasema ofisi yake tayari imefuta ushirika wa G32 kwenye daftari la Serikali la vyama vya ushirika hivyo ushirika huo hauna nafasi ya kusikilizwa wala kuendelea kuwepo na kuendelea na shughuli zake.
Kwa muda mrefu Mrajisi msaidizi Mkoa wa Kilimanjaro John Henjewele amekuwa akisumbuana na ushirika huu wa G32, na kufikia hatua hadi ya kuingia biashara ya kahawa ya kilimo hai kwa wanachama wake baada ya kuona ushirika huo umekuwa kikwazwa kushindwa kuifufua KNCU.
Nilisoma habari iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku juu utetezi uliotelewa na G32 baada ya uamuzi wa Mrajisi, nikapata mashaka kwani licha ya uongozi kuomba kupewa nafasi ya kusikilizwa juu ya kufutwa kwa ushirika wao na kuomba kupewa muda kumalizia kuuza kahawa waliyonayo bado hawajapewa nafasi hiyo.
Mimi kama mkulima kwa uelewa wangu mdogo tu najua kwamba ushirika ni hiari sasa inakuwaje Serikali iingilie ushirika ambao umeanzishwa na wakulima huku ukiwa umesajiliwa kisheria leo unaamka tu na kusema kwamba unafuta ushirika huo.
G32 KNCI ulibuniwa baada ya sheria ya ushirika na ile ya kahawa kubadilika mwaka 1994 ambayo iliruhusu soko huru la kahawa ambapo wakulima wanaweza kuuza kahawa yao kupitia ushirika au makampuni binafsi.
Wakati mrajisi anafikia uamuazi wa kuifuta G32 wakifikiri kwamba ndio njia ya kufufua KNCU wanasahau kwamba bila G32 vyama vya ushirika vingekuwa vinataabika kwani KNCU haijafanya biashara ya kahawa kwa miaka 3 huku ikiwa na madeni makubwa yaliyopelekea kuuza mashamba,nyumba huku ikiwa na madeni makubwa kwa vyama.
Wakati Serikali ikiruhusu soko huru la kahawa KNCU haikuwa imejiandaa kwa hili kwani ilikuwa ikiendesha biashara ya kahawa kwa mazoea huku ikiwapoka wakulima wanapopeleka kahawa yao chamani.
Kama ushirika ni hiairi mrajisili anatoa wapi mamlaka ya kufuta ushirika wa G32 ambao hauna malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima wanchama na kuacha kuhangaika na changamoto za KNCU ikiwemo madeni ya muda mrefu kwenye vyama vya ushirika, ambayo yalifanya vyama hivyo kujiondoa KNCU.
Kwa sasa ushirika huo unaolazimishwa vyama kujiunga kwa nguvu bado upo kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi, baadhi ya vitega uchumi vyake vipo taabani kama Hoteli maarufu ya KNCU ambayo ilifahamika kama coffee tree hapo zamani ambayo kwa sasa imefungwa kwa kushindwa kujiendesha.
Ni mkulima yupi wa kahwa mkoani Kilimanjaro asiyejua ubadhirifu chama hichi kikuu, madeni makubwa yaliyopelekea kuuza maliza zake kama mashamba,nyumba,magari hali ambayo imepelekea kushindwa kufanya biashara ya kahawa na kuishia kuwakopa wakulima.
Wakulima wanaumia wanapoona uamuzi huu wa Mrajisi kufungia ushirika ambao yeye mwenyewe aliusajili. wakati wanafungia G32 ina kahawa ya kilimo hai (organic cofee) yenye dhamani ya tsh milioni 500 ambayo tayari ina wateja nje ya nchi na inatakiwa kuuzwa.
Lakini pia kwa muda mrefu ambao KNCU imeshindwa kufanya biashara ya kahawa G32 ndio imekuwa msaada mkubwa,ikiwemo kupigania kurejeshwa kwa mali za KNCU ambazo ziliuzwa kinyemela na viongozi wake.
G32 ambayo ilisajiliwa mwaka 2008 haijapewa nafasi ya kusikilizwa baada ya uamuzi wa kufutwa mbapo wakati uamuzi huo unafanyika ushirika huo tayari umekusanya zaidi Kg 19,425 za kahawa ya wakulima ambayo wanapewa maelekezo ya kukabidhi KNCU.
Mrajisi anasahau kuwa KNCU imekuwa na malalmiko ya muda mrefu kwa wakulima kwa kushindwa kutoa huduma,je kahawa hiyo wanaikabidhi KNCU kwa makubaliano gani wakati bado wakulima wanadai fedha za miaka nenda rudi mpaka leo hawajalipwa.
Uamuzi wa Mrajisi hauzingatii kwamba G32 Walikuwa na mikataba ya mauzo ya kahawa nje, haijali, ilikuwa na mkopo haijali, uamuzi ni kwamba Serikali imeamua kufuta ushirika ili kufufua KNCU.
Kama Mrajisi anaona uwepo wa G32 unaathiri shughuli za KNCU au kufuta G32 ni njia ya kufufua KNCU mbona makampuni binafsi yameruhusiwa kununua kahawa kwenye vyama vya msingi na kushiriki minada na hata kusafirisha nje kosa la G32 hapa ni lipi?
Ni dhahiri kwamba Rais Dkt John Magufuli anafanya kazi kubwa sana ila nadiriki kusema baadhi ya watendaji wake wanamuangusha jiulize unafuta ushirika wa wakulima ambao umesajiliwa kisheria ,kisha unatoa maelekezo kahawa waliyonayo na mali wapeleke kwenye ushirka mwingine Je kama mteja atakataa kununua kahawa hiyo kwenye taasisi nyingine ni nani atawajibika kwa hasara itayotokea?
Iweje useme unafuta ushirika kwa sababu unafanya shughuli zinazofanana na KNCU licha ya kwamba kuna makampuni binafsi ambayo yanafanya shughuli zinazofanana na KNCU za kununua kahawa kwenye vyama vya msingi na hata kufanya Direct Export je hii inaingia akilini ni uonevu.
Kwamba wanachama wa G32 pia ni wanachama wa KNCU,hivyo ndo sababu ya kufuta ushirika wa G32 licha ya kusahau kwamba kanuni ya 29(1) ya vyama vya ushirika inaruhusu uanachama pacha kama ambavyo nimeeleza huko juu kwamba ushirika ni hiari.
Masuali tunayojiuliza kama wakulima leo Serikali imefuta usajili wa ushirika tuliounda kwa hiari yetu inatulazimisha kujiunga na KNCU je hiyo ndiyo dhana ya ushirika ina lengo la kuhakikisha ushirika unakufa KIlimanjaro,sababu kama sisi wakulima tunaozalisha kahawa ya kilimo Hai, tunajua KNCU haina leseni ya kuuza kahawa ya kilimo hai nje ya nchi hivyo tunaokuwa wahanga wakubwa wa maamuzi haya ni wakulima.
Mrajisi tunakubali wewe ndiyo msimamizi wa ushirika nchini lakini KNCU tumeianzisha sisi tunaijua mpaka sasa KNCU haikopesheki,ina madeni makubwa,vyama vya msingi vina madai ya muda mrefu baada kufanya baishara na union ambapo wakulima sisi ndo tunaumia hatujaona jitihada yako kwenye hili zaidi kuingilia na kufuta ushirika ambao umekuwa ni msaada mkubwa kwetu.
Hivi Mrajisi una kumbukumbu kwenye ofisi yako kwamba KNCU ilishindwa kabisa kufanya biashara ya kahawa tangu msimu wa 2016/2017.
Vipi Kiwanda cha kukoboa kahawa cha TCCO Ltd ambacho kilikuwa taabani, ushirika wa G32 ndio imekuwa mteja wake mkubwa kwani kwa muda mrefu vyama vya msingi vimekuwa vikikobolewa kahawa yao kwenye viwanda binafsi.
Kama ilivyo dhana ya ushirika kuwa ni hiairi maamuzi ya Mrajisi yana madhara makubwa kama yafuatayo endapo uamuzi huu hatubatilishwa na Serikali kwani maamuzi ya kufutwa G32 haujaangalia adhari kwa wana ushirika wenyewe ambavyo ni vyama 32, vya msingi vilivyopo Mkoani Kilimanjaro, ambao wanamiliki mali kadhaa na hata fedha zaidi ya milioni 117 zitakuwa mashakani na wanachama hawajui hatima yao mpaka sasa.
Itakumbukwa kuwa wakati Serikali ikirejesha mali zilizouzwa na baadhi ya viongozi kinyemela hivi karibuni zaidi ya Bil 2, mwaka 2015 G32 ilisimama kidete kupinga uuzwaji huo wa mali hadi kupelekea tume maalumu ya ushirika kuundwa sasa tunajiuliza Mrajisi hatambui mchango wa G32 ani ni ni mipango ya kuufuta ili waendeleze madudu yao?
Ni mimi Mkulima Mzalendo
Kilimanjaro