Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Majuzi kuna mdau aliweka uzi kuhusu mitungi ya gesi kugaiwa kwa masharti ya kutoa namba ya nida - Nzega, Tabora: Mtaani kwetu kuna watu wanapita Kila kaya wanagawa mitungi ya gesi, Sharti lao uwape namba yako ya NIDA
Tunajua taarifa za nida zinatumika sehemu nyingi ikiwepo na kwenye vitambulisho vya kupiga kura, ukiwa na namba ya nida ya mtu ina maana una taarifa zake zote za kutosha kuandaa kitambulisho kingine.
Kwanini hakuna utaratibu mwingine wa kuhakikisha kuwa sehemu fulani imefikiwa mpaka wachukue namba ya NIDA? Kwanini wasitumie wajumbe mtaani wanaojua watu wote kwenye mitaa yao kufanikisha zoezi hilo?
Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao nao wanagawa mitungi ya gesi, je, pia nao wanadi namba ya NIDA? - Pre GE2025 - Mama Ongea na Mwanao kugawa mitungi ya gesi
Zoezi hili kuendeshwa wakati huu tena makundi mbalimbali ya CCM kuhusika ni rushwa ya wazi wazi kipindi cha uchaguzi.
Huu ni ubabaishaji unaanza kutengenezwa mapemba kabisa na kuja kutuletea takwimu ambazo hazina uhalisia.
======
Akijibu swali aliloulizwa kuhusu utaratibu wa kugawa mitungu ya gesi leo Februari 10, 2025, Naibu Waziri Wizara ya Nishati Ndg. Judith Kapinga amesema;
"Kwa utaratibu wa sasa hivi kila mtungi mmoja unaenda kwa kwa mtu mmoja na inachukuliwa vile vile kwa namba ya nida yote ni kuhakikisha tunaweza kufikisha mitungi kwa wananchi wengi zaidi.... na kwenye kila mkoa kuna mawakala.."