Serikali kuichunguza hospitali iliyothibitisha kifo cha bibi ambaye baadaye alijulikana yupo hai

Serikali kuichunguza hospitali iliyothibitisha kifo cha bibi ambaye baadaye alijulikana yupo hai

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Serikali ya Ecuador imeanza kuichunguza hospitali aliyokuwa akitibiwa bibi mmoja ambaye alitangazwa amekufa lakini aliamka ndani ya jeneza Ijumaa iliyopita.

Bella Montonya (76) ambaye madaktari walithibitisha kifo chake aligundulika yupo hai baada ya mtoto wake kusikia kelele zikitokea kwenye jeneza wakati wa maandalizi ya mazishi.

Bibi huyo alikuwa akigongagonga ndipo walipoenda kutizama na kumkuta akiwa anapumua kwa nguvu, walimtoa na kumkimbiza hospitali huku waombolezaji wakibaki na mshtuko mkubwa.

Kamati maalumu imeundwa kupitia upya mchakato unaofanywa na hospitali za nchini humo mpaka kutoa cheti cha kifo.
 
Back
Top Bottom