Serikali kuingilia kati sakata la Simba SC na FCC

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Baada ya wabunge kuchachamaa bungeni wakitaka kujua lini sakata la Simba na FCC litakwisha ili mambo yaendelee hatimaye majibu yapatikana, sasa majibu kupatikana jumatatu.
===
Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema vikwazo vilivyoibuka katika uwekezaji wa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ katika klabu ya Simba huenda vikamalizika Jumatatu Aprili 19, 2021 wakati Tume ya Ushindani (FCC) itakapokutana kwa mara ya tatu na pande zinazohusika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa leo Ijumaa Aprili 16, 2021 bungeni mjini Dodoma baada ya mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi kutaka kushika shilingi wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya ofisi ya waziri mkuu mwaka 2021/22.

Shangazi aliitaka Serikali kumaliza ukiritimba kwenye uwekezaji nchini, akiutolea mfano uwekezaji wa Mo Dewji katika klabu hiyo kongwe nchini akisema wanaicheleweshea Simba kufikia kwenye mafanikio.

Mbunge huyo amesema hakuna sheria maalum inayoongoza uwekezaji katika sekta ya michezo, bali sheria inayotumika ni ya Baraza la Michezo (BMT) aliyodai ina upungufu na kuhoji ni lini Serikali itawasilisha bungeni sheria hiyo ili kumaliza mvutano.

Hoja hiyo ilitolewa ufafanuzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Geofrey Mwambe, “kilichotokea ni kwamba zilikwenda kampuni nne na mwekezaji mmoja, baada ya hapo FCC ilibaini upungufu katika mchakato mzima.”

“Tume iliagiza klabu ya Simba ijibu dosari zilizojitokeza, lakini baada ya hapo wakaenda mahakamani baadaye wakakubaliana waondoe kesi mahakamani na kurejea meza ya maridhiano, jambo ambalo linaendelea hata sasa.”

Alibainisha kuwa Serikali inafuatilia kwa karibu kuona mgogoro huo unakwisha kwa manufaa ya maendeleo ya michezo na uwekezaji nchini.

Hata hivyo, Shangazi alisimama na kusema wanachokililia wabunge ni sera ya uwekezaji ambayo itaondoa ukiritimba huo.
Kauli hiyo ya Shangazi ilimnyanyua Bashungwa na kubainisha kuwa ipo fursa ya uwekezaji katika sekta ya michezo na sheria namba 18(a) inabanisha kwamba mtu anaweza kuwekeza kwenye timu ya michezo kwa kiwango kisichozidi asilimia 49 ya hisa na kwamba ndicho kilichozingatiwa katika uwekezaji kwenye klabu hiyo.

Bashungwa amesema FCC na Simba watakutana kwa mara ya tatu Jumatatu ijayo na Serikali inaamini utakuwa mwisho wa mvutano wa uwekezaji ndani ya klabu hiyo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumzia suala hilo amesema ni vema jambo hilo likamalizwa haraka kwa maelezo kuwa haiwezekani klabu kubwa inayojiandaa na mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kukwamishwa kwa jambo dogo lililochukua miaka mingi.


CREDIT: THE CITIZEN
 
simba kujadiliwa bungeni ni kitu ya kawaida, maprofesa uchwara watatoa wapi KIKI?
 
FCC kinawauma nini?
Wakamilishe mchakato hela zimwagwe uwanjani
 
Reactions: mmh
siasa zisiingilie huo mchakato ni heri wakaacha FCC wafanye kazi yao kwani mara nyingi maamuzi ya siasa yanategemea upepo wa kiongozi aliyepo madarakani.

Kama watapitisha maamuzi ya kisiasa wajue mbeleni yatatenguliwa ila kama watapitisha maamuzi ya kisheria utawala wowote utakaokuja utaheshimu hayo maamuzi.
 
Kwa Hiyo FCC kazi yao kubwa ni kukwamisha tu juhudi za wenzao! Halafu utakuta mkurugenzi wake anapiga na bia kabisa huku kazi haziendi, bongo bana!

Kama wanachanganya mapenzi na kazi hii nchi hatutaki longolongo. Kodi zinalipwa. Ajira zinatengenezwa. Biashara inafanyika.
Yaani ukiendaga viwanjani siku za mechi huwa kuna biashara kubwa na nyingi lakini mafcc hayaoni sijui yanaishi wapi. Mpaka hapo walipofikia inatakiwa mkurugenzi wake atumbuliwe na kesi ya uhujumu uchumi, anahujumu uchumi wa nchi.

Wao hawaoni kifuani pale kuna visit Tanzania? Sasa hapo nani anasaidia nchi. Mama samia fumua pale pale, kuna Mungu watu pale.
Kama kuna dosari lengo liwe kurekebisha lakini wao naona wana lengo la kukwamisha kwa kujidai kuna dosari.

Mama mama mama japo uko kwenye mfungo ila kuna watu wanakuchokonoa huku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…