Serikali Kujenga Shule 56 za Michezo Nchi Nzima, Kila Mkoa Kupata Shule Mbili

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI KUJENGA SHULE 56 ZA MICHEZO NCHI NZIMA, KILA MKOA KUPATA SHULE MBILI

Akijibu swali namba 559 la Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro; Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali ina mpango wa kujenga Shule 56 za Michezo nchini ili kukuza, kulea na kuendeleza vipaji vya vijana.

"Serikali inayo mikakati mbalimbali ya kuwezesha wadau wake kuwekeza katika kuzalisha vipaji vya michezo hususani mpira wa miguu ikiwemo kuandaa miongozo na kanuni mahususi zinazowalinda wadau wanaoanzisha Shule Maalum za kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo (Sports Academies) ili kuhakikisha wananufaishwa na uwekezaji wanaoufanya" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro

"Pamoja na hatua kadhaa nyingine, Serikali inawaunganisha wadau hao na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia program kadhaa za kuibua na kuendeleza vipaji zikiwemo UMITASHUMTA, UMISETA na UMISAVUTA"

"Serikali imeanzisha mafunzo ya elimu ya michezo ngazi ya Astashahada na Stashahada katika Vyuo Sita nchini ikiwemo Vyuo vya Ualimu Butimba, Korogwe, Mpwapwa, Monduli na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya"

"Serikali inaendelea Kuimarisha utoaji wa mafunzo ya Shahada ya kwanza katika elimu ya michezo kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza idadi ya wataalamu wa kufundisha michezo ili kupunguza gharama za uwekezaji"

"Serikali imejipangaje kuendeleza vipaji vya vijana hao? Serikali ina mpango gani wa kujenga na kuboresha viwanja vya michezo mashuleni na kwenye Vyuo?" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Serikali kwa kushirikiana na TFF tunaandaa mashindano mbalimbali ya vijana ili vipaji ambavyo vimeweza kupatikana viweze kukuzwa na kuendelezwa kupitia mashindano hayo"

"Kuna Ligi ya Chini ya Miaka 17 (U17), tuna UMISETA, UMITASHUMTA. Mashindano hayo yote yana lengo la kuhakikisha kwamba vipaji vinavyopatikana vinaweza kuendelezwa. Katika Kituo cha TFF Tanga na Dar es Salaam mafunzo ya kuendeleza vipaji yanaendelea"

"Bajeti tuliyopitisha tarehe 23 Mei ya Mwaka 2024/2025 tulisema Serikali ina mpango wa kujenga Shule 56 ili kuzibadirisha kuwa Shule za Michezo ambazo zitakuwa ni Shule 2 kwa kila Mkoa Tanzania Bara na Visiwani zitakuwa ni mahususi kuchukua vipaji na kuviendeleza na kuendeleza miundombinu ya michezo katika Shule hizo" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 
Attachments

  • WhatsApp Video 2024-06-07 at 11.04.16.mp4
    23.1 MB

SERIKALI KUJENGA SHULE 56 ZA MICHEZO NCHI NZIMA, KILA MKOA KUPATA SHULE MBILI

Akijibu swali namba 559 la Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro; Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali ina mpango wa kujenga Shule 56 za Michezo nchini ili kukuza, kulea na kuendeleza vipaji vya vijana.

"Serikali inayo mikakati mbalimbali ya kuwezesha wadau wake kuwekeza katika kuzalisha vipaji vya michezo hususani mpira wa miguu ikiwemo kuandaa miongozo na kanuni mahususi zinazowalinda wadau wanaoanzisha Shule Maalum za kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo (Sports Academies) ili kuhakikisha wananufaishwa na uwekezaji wanaoufanya" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro

"Pamoja na hatua kadhaa nyingine, Serikali inawaunganisha wadau hao na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia program kadhaa za kuibua na kuendeleza vipaji zikiwemo UMITASHUMTA, UMISETA na UMISAVUTA"

"Serikali imeanzisha mafunzo ya elimu ya michezo ngazi ya Astashahada na Stashahada katika Vyuo Sita nchini ikiwemo Vyuo vya Ualimu Butimba, Korogwe, Mpwapwa, Monduli na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya"

"Serikali inaendelea Kuimarisha utoaji wa mafunzo ya Shahada ya kwanza katika elimu ya michezo kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza idadi ya wataalamu wa kufundisha michezo ili kupunguza gharama za uwekezaji"

"Serikali imejipangaje kuendeleza vipaji vya vijana hao? Serikali ina mpango gani wa kujenga na kuboresha viwanja vya michezo mashuleni na kwenye Vyuo?" - Mhe. Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro

"Serikali kwa kushirikiana na TFF tunaandaa mashindano mbalimbali ya vijana ili vipaji ambavyo vimeweza kupatikana viweze kukuzwa na kuendelezwa kupitia mashindano hayo"

"Kuna Ligi ya Chini ya Miaka 17 (U17), tuna UMISETA, UMITASHUMTA. Mashindano hayo yote yana lengo la kuhakikisha kwamba vipaji vinavyopatikana vinaweza kuendelezwa. Katika Kituo cha TFF Tanga na Dar es Salaam mafunzo ya kuendeleza vipaji yanaendelea"

"Bajeti tuliyopitisha tarehe 23 Mei ya Mwaka 2024/2025 tulisema Serikali ina mpango wa kujenga Shule 56 ili kuzibadirisha kuwa Shule za Michezo ambazo zitakuwa ni Shule 2 kwa kila Mkoa Tanzania Bara na Visiwani zitakuwa ni mahususi kuchukua vipaji na kuviendeleza na kuendeleza miundombinu ya michezo katika Shule hizo" - Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo
Asilimia 90 ya shule zote nchini zinapaswa kuwa za michezo!
 
..sio kwamba kila shule inatakiwa iwe na waalimu wa michezo, sanaa, etc etc

..nchi ambazo zimeendelea na zimefaulu ktk michezo, je, wana " academy " za michezo?

..kwa mfano, Kenya, na Ethiopia, wamefaulu sana ktk riadha. Je, wamefaulu kwa kuanzisha "academy"?
 
Back
Top Bottom