Pre GE2025 Serikali kujenga uwanja mpya wa ndege Kagera

Pre GE2025 Serikali kujenga uwanja mpya wa ndege Kagera

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kufatia kuwepo kwa mahitaji makubwa ya uwanja mkubwa wa Ndege, mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameridhia kutoa fedha za ujenzi wa uwanja mpya wa Ndege katika maeneo ya Kyabajwa wilayani Missenyi.

Akitoa taarifa hiyo kwenye kikao cha bodi ya Barabara mjini Bukoba Mwassa amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo umezingatia mahitaji makubwa ya usafiri wa anga ambao umekuwa ni masha ya watu wa Kagera sambamaba na urahisishaji wa usafirishaji wa mizigo mikubwa tofauti na sasa ambapo ndege kubwa haziwezi kutua.

Soma pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha amewaomba wananchi wa Kagera kutoanzisha malumbano na migogoro yenye lengo la kukwamisha mradi huo sambamba na kueleza kuwa mradi wa ukarabati wa bandari za Kemondo na Bukoba umefikia hatua nzuri na sasa Meli kubwa zitaana kutia nanga.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Rweikiza ameishukuru serikali kwa ujenzi wa uwanja huo ambao unakwenda kufungua fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi kwa wananchi wa Kagera.

Ameongeza kuwa ujenzi wa uwanja huo uende sambamba na ujenzi wa Daraja la Kansinda ambalo litarahisisha mawasiliano kwa wananchi kwakuwa ni maeneo ambayo yapo karibu na eneo unapokwenda kujengwa uwanja wa Ndege.

 
Hii ina maana haitokuwa tena omukajunguti, na baadala yake ni Kyabajwa. Je hii itakuwa chachu ya kuinua mandeleo ya wilaya Missenyi ambao kwa asilimia kubwa wakazi wa Missenyi wamekuwa wakifuata baadhi ya huduma Bukoba manispaa?
 
Back
Top Bottom