Serikali Kukarabati Madaraja Yaliyoharibiwa na Mvua

Serikali Kukarabati Madaraja Yaliyoharibiwa na Mvua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI KUKARABATI MADARAJA YALIYOHARIBIWA NA MVUA.

Naibu Waziri, Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa -TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali inatambua umuhimu wa miundombinu ya Madaraja na inaendelea na urekebishaji wa madaraja yote ambayo yaliharibiwa na mvua zilizomalizika.

Mhe.Katimba ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu wakati akijibu swali la mheshimiwa Anna Richard Lupembe mbunge wa jimbo la Nsimbo ambaye aliuliza Je, lini Serikali itajenga Daraja la Mafunsi Kata ya Itenka – Nsimbo.

Amesema kutokana na mvua za mwaka 2023/24 Wakala unapitia usanifu uliofanyika ili kujiridhisha kutokana na hali ya wingi wa maji uliobainika kwenye kipindi cha mvua za elinino. Kazi ya kupitia usanifu inaendelea kukamilishwa na inatarajia kukamilika mwezi wa Septemba, 2024 na mara itakapokamilka taratibu za ujenzi zitafuata.

Mheshimiwa Katimba ameongeza kuwa Serikali inafahamu umuhimu wa ujezi wa Daraja la Mafunsi Kata ya Itenka – Nsimbo, mwaka 2023/24 daraja hili lilifanyiwa usanifu ambapo gharama zinazohitajika zilikuwa Shilingi bilioni 2.3.
IMG-20210524-WA0168.jpg
GWObkhEWcAAm-9L.jpg
GWObkhIXQAA5gge.jpg
GWObkg-WMAASf8h.jpg
GWObkhIXkAAM08T.jpg
 
Back
Top Bottom