Serikali kukodi ndege ya mizigo kupeleka maua, samaki nje

Serikali kukodi ndege ya mizigo kupeleka maua, samaki nje

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Serikali imesema itakodi ndege kupeleka matunda na mbogamboga nje ya nchi kutoka katika viwanja vya ndege vya Songwe na Mwanza, wakati huu ikijiandaa kununua ndege ya mizigo kwa kazi hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema). Katika swali lake, Selasini alisema Mkoa wa Kilimanjaro na hasa Wilaya ya Rombo ni wakulima wazuri wa parachichi, lakini matunda hayo yanapelekwa kwa wingi nchi jirani ya Kenya na kusafirishwa kwenda ughaibuni, kwa nini serikali isinunue ndege ya mizigo kwa kazi hiyo.

Kamwelwe alisema kwa sasa serikali inaitumia ndege ya KLM kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kubeba mazao hayo kila siku kwenda Ulaya. Alisema kutokana na hali hiyo kwa sasa serikali itatumia kukodi ndege katika viwanja vya Mwanza na Songwe kwa ajili ya kubeba minofu na mazao kama parachichi kupeleka Ulaya.

Alisema soko la bidhaa kutoka Tanzania kwenda Ulaya ni kubwa, lakini la kutoka Ulaya kuja Tanzania bado ni dogo, hivyo wataendelea kukodi wakati mpango wa kununua ndege ya mizigo ukiendelea kufanyiwa kazi.

Akijibu swali la nyongeza, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema hivi sasa serikali inaandaa sheria ya kuunda mamlaka ya kusimamia mazao ya mbogamboga na matunda ambayo itafanya kazi ya kusimamia sekta hiyo yakiwamo mazao ya parachichi. Alisema sheria itatungwa hivi karibuni ya kuwa na mamlaka hiyo, na kwa sasa baadhi ya matunda hayo yanasafirishwa kwa njia za anga na bandari kwenda nje.

Chanzo: Habari Leo
 
Nzuri japo ina ukakasi!

Tunaongelea zaidi parachichi sasa kwa sababu Kenya wamepata deal kubwa ya bidhaa hizo China na Ulaya. Pia issue za maua Kenya ndio imezishika kwanye ukanda huu ndio maana hata wakulima wa Uganda na Tanzania huenda 'wanawauzia' Kenya kwa maana ndio wana contacts nzuri za wanunuzi then wakishayapeleka Ulaya yote yanakuwa branded kama ya Kenya.

Hii kitu huwezi kuibadilisha kwa kununua ndege au kukodi maana serikali kama serikali haina shamba la mboga, parachichi ama maua na haifanyi biashara hiyo.

Cha msingi hapa ni kuwapa uwezo wafanyabiashara (middlemen) na wakulima wa mazao husika ili wazalishe kwa urahisi na waweze kuyafikia hayo masoko na hapo linaweza kuwa wazo endelevu lakini si kukodi tu ndege.

Muuzaji akishapata uhakika wa soko kinachobaki ni delivery tu na hiyo linafanya shirika lolote la ndege na wakifanikiwa zaidi watakodi ndege zao au hata kununua za kwao kama Precision!
 
Antonov kule Urusi zipo kibao tu hazina wanunuzi na bei ndogo kabisa, tuache uoga na ujinga tufungue bongo zetu. Juzi pm alikuwa urusi alishindwa hata kuliona hili na wasaidizi wake hata tukope antonov cargo plane 4 za tani 30 kila moja halafu tukazikabidhi shirika la posta zikawa zinatumika na posta na zikapigwa chapa tanzania courier service. Kila siku kukawa na trip za tanzania-guanzhou halafu muone kama zitakosa mizigo.

Hizi landlocked zote hazina samaki wa baharini wala tilapia, beba samaki kila siku peleka Kigali, Kampala, Lusaka, Lilongwe, Lubumbashi, peleka pia tilapia pale Namibia na Harare. Pale London lipo soko kubwa la tilapia hawa beba peleka kila siku asubuhi fresh one halafu ndani ya mwaka muone pato lake.

Tanzania ni shamba lenye fursa nyingi sana ambazo duniani huko zinahitajika sana ila tatizo tumekosa vichwa vyenye uwezo wa kuongoza hawa milioni 50 plus kwenda mbinguni, watanzania sio watu wakuwa masikini kabisa kama kweli wenye mamlaka wataweza kufikiri, nina uhakika watanzania mamilioni kwa mamilioni wangekuwa matajiri.
 
lukindo, Well said mkuu. Sijui kwanini Serikali za Kiafrika hazipendi kuwajengea uwezo watu wake ili waweze kutrade worldwide badala yake ni blah blah za kisiasa tu. Ukiangalia paragraph zako mbili za mwisho zimebeba ujumbe mzito sasa ambao ndio unafanya leo hii tunawaona wazungu wafalme duniani hapa.
 
samurai, Ni wazo pia, wamarekani huwa wanasema 'talk the talk....'. Hizi fursa unazoziongelea hapa kuna watu wanazijua pia lakini daima 'know how' ndicho kigezo kikuu cha kumbadilisha binadamu.

Mfano nilikuwa naangalia habari leo, Hong Kong ni sehemu ya china lakini miaka ambayo walitawaliwa na waingereza akili zao ni tofauti kabisa na China-mainland! Ndio maana nchi kama Sweden idadi yao ni milioni 10 lakini kwa sababu wamepewa misingi mizuri na sahihi ya kufikiri wanaweza kutusaidia sisi tulio milioni 60 na rasilimali zote tunazo!

Hiyo mifano huenda ikatutoa kwenye hoja lakini unavyotaka kusema ni kuwa ukiona nyanya zimemwagwa polini huko Gairo na ndoo inauzwa 1,500/- alafu ukawaza Dasr es Salaam nyanya 4 zinauzwa 1,000/- ukaconclude kwa kununua fuso ili uzisombe kuzileta sokoni ujue wazi kuwa unatakiwa kurudisha milioni zaidi ya 60 za kuinunua hiyo Fuso na faida juu! Pia ujue hapo sokoni wapo madalali na vitu vingine visivyoelezeka.
 
lukindo, Mkuu point yangu ya msingi ipo kwenye kuwajengea watanzania uwezo wa kufanya biashara wenyewe kimataifa na sio kukimbilia kwenye mambo makubwa huku msingi haupo na mwisho wa siku tukakwama.

Wakenya wanatuacha mbali sana kwa sababu jamii yao imechangamka kichwani na ule uwezo wao wa kupambana kimataifa ndio umeleta wawekezaji na kuleta connection kwao kiasi cha kuweza kufanya biashara kimataifa. Angalia wanyarwanda wanavyokuja kasi, sababu ni ile ile usmart kwenye vichwa vya watu.. Hapa ni muhimu sana kuwapa watu Elimu iliyo bora na kujenga utamaduni unaoendena na dunia ya sasa na tuachane kabisa na akili za kijamaa

Ukiwa pale Jomo Kenyata International Airport utaona madege mengi ya mizigo kuanzia Fedex, Aramex mpaka DHL yanaleta na kubeba mizigo, kwahiyo hapa utaona issue kumbe sio kuwa tu na ndege bali kuwepo tayari na watu wa kutosha wenye uwezo wa kufanya biashara pande zote za dunia.

Mfano tukiwa na watanzania tayari wana connection na uwezo wa kuchukua samaki kila asubuhi kilwa na kupeleka Lubumbashi tayari hapa mahitaji ya ndege yatakuwepo na zitakuja tu. Ndege za mizigo zinakwenda Kenya kwa wingi kwasababu upo uhitaji wa ndege kwenda.
 
Hi ndege ya muhimu sana tuuze hata dreamliner moja tununue hiyo ndege
 
Tungekuwa na plan na mission na mission tusingejaza midege nane ya abiria huku tukiwa
Hatuna hata moja ya huduma za dharura na majanga
Hatuna hata moja ya mizigo mizito na ya kati
Hatuna hata moja ya ambulance/fire []chopper []
 
Back
Top Bottom