benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuendeleza mchezo wa Soka nchini itamlipa mshahara mwalimu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Adel Amrouche ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria.
Hayo yamebainishwa wakati wa kumtambulisha Kocha huyo, Machi 07, 2023 Mtumba jijini Dodoma na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali inaamini Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limejiridhisha kuwa ni Kocha Bora atakayekuza soka la Tanzania.
Dkt. Chana ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuangalia uwezekano wa kupata Wataalamu katika michezo mingine ambapo ameeleza kuwa Wizara inaendelea kuimarisha Wataalamu wa michezo kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Kwa upande wake Kocha Amrouche ameahidi kuwanoa wachezaji vyema ili kuiweka juu zaidi Tanzania katika ulimwengu wa Soka , huku akisisitiza ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali katika kufanikisha kazi yake.