Serikali kuongeza kodi ya mafuta na kushusha ya vinywaji ni sawa na Muuaji anayetabasamu

Serikali kuongeza kodi ya mafuta na kushusha ya vinywaji ni sawa na Muuaji anayetabasamu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Anapotokea mtu akapandisha kodi ya Mafuta akashusha kodi ya Vinywaji na wananchi wakaridhika inaonesha ni jinsi gani tuna taifa la kinafiki kwa kiwango kikubwa.

Kuna wale wauaji ambao huwa wana sura za upole na hawajengi makunyanzi wakati wakitaka kutimiza malengo yao.

Hawa wanaweza kukubembeleza kuwalaza shingo hapa, laza baba/mama eeeeenheeh laza taratibu usiumie. Weka vizuri shingo yako ili nikipiga panga nisiguse kichwa chako" Huku anakukanda kanda shingoni na kukutomasa tomasa, ukija shtuka ameshusha panga. Umekufa.

Serikali ya kijambazi inaongeza kodi/mzigo kwa wananchi pasipo kuwajali wataishije. Unapoongeza kodi kwenye mafuta unaathiri wananchi wote kuanzia wakulima, wafugaji hadi wafanya biashara.

Mwanachi huyu huyu unamwongezea kodi kwenye matumizi yake ya simu na bado unakuja mpa mzigo mwingine kwenye mafuta. Sisi ni wendawazimu. Sisi ni matahira. Tunanyamaza.

Hawa wanaongeza kodi magari wanayotumia tunawalipia sisi mafuta hawana hasara. Tupambane katika hili. Huu ujambazi wa Serikali upigiwe kelele.
 
Hivi kodi ya 1,000 kwa mwezi kwenye laini za simu inaanza lini?
 
CCM ni ile ile kwa hiyo tusitarajie maajabu kwa huyu ustadhati! Ni yale yale tu 'like father like mother'!
 
..."ukija kushtukia panga limeshuka,umekufa"...!Hahahaaa!Unaamka unamwambia "kili me softly,kaka jambazi"!😝😝😝😝😝😝
 
Sisi wananchi ni wapumbavu sijapata kuona!

Wakati Mwigulu anasoma bajeti ya nchi kule bungeni mambo yalikuwa hivi: [emoji116]

Uzi wa bajeti ulikuwa na coments 90

Uzi wa Sabaya ulikuwa na coments elfu 1 na zaidi

Uzi wa kusaini petition ya kumtoa Diamond kwenye tuzo za BET ulikuwa na coments 800 na zaidi

Acha kodi ipande hata mara 20!
 
Mama hapa kwenye mafuta kachemka. Wapiga dili naona wanaanza mdogo mdogo.

Mafuta yakipanda kila kitu kitapanda nadhan mda si mrefu mikoani mafuta yatafika 3000.
 
Back
Top Bottom