Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwa wale watumishi wa umma ambao taasisi zao huwalipa posho kila mwezi(mfano JWTZ, Polisi, n.k), wakati umefika waruhusiwe kukopa kupitia posho hizo kwa kukatwa sehemu ya posho zao kulipa mikopo watayochukua.
Tofauti na mikopo kupitia mishahara ambayo huwa ni ya muda mrefu (miaka 7 mpaka 8), mikopo kupitia allowance za kila mwezi, inaweza kuwa ni ya muda mfupi (mfano miezi 6 mpaka miaka 2).
Hii ni kwasababu, mishahara serikalini ni midogo na wakati huo huo, watumishi wananabwa na sheria inayowataka wabaki na walau moja ya tatu ya mishahara yao baada ya makato yote yakiwemo makato ya lazima kama Bima na ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Matokeo ya hali hii ni watumishi kupata mikopo midogo isiyolingana na mahitaji yao, na kuwafanya wengi kukimbilia katika microfinance ambazo licha ya kutowapa mikopo mikubwa, bali hutoa mikopo yenye riba kubwa na hata kufanya ile dhana ya mtumishi kubaki na moja ya tatu kuwa ni nadharia tu kwani mtumishi hulazimika kutumia mshahara huo huo kulipa mikopo ya mabenki na ya hizi financial institutions.
Hivyo, kwa wale watumishi wanaoweza kukopa kupitia posho zao za kila mwezi ambazo nazo hulipwa kupitia akaunti zao katika mabenki, wakati umefika waruhusiwe kukopa mikopo ya muda mfupi kupitia allowance zao za kila mwezi.
Tena, kama inawezekan, mtumishi aruhusiwe kutumia mshahara na allowance yake vyote kwa pamoja kupata mkopo na kwenye allowance, mtumishi aruhusiwe hata kukopea allowance yote mradi kaamua mwenyewe.
Mfano, mtumish ana allowance ya shilingi 300,000 kwa mwezi, na kupitia mshahara wake, anaweza pia kutumia shilingi 200,000 kukopea, maana yake mtumishi kama huyu, akiamua, anaweza kutumia shilingi 200,000 ya posho na hiyo 200,000 ya mshahara wke akapata jumla ya shilingi 400,000 kwa mwezi, kiasi anachoweza kwenda Benki na akachukua mkopo wa muda mfupi na akapata hela nzuri tu na akafanya mambo yake?
Jambo hili mimi naamini linawezekana iwapo serikali kupitia BOT, Utumishi na mabenki, watakaa pamoja na kulifanyia kazi wazo hili.
Watumishi wengi kwa sasa hawakopesheki katika mabenki kutona na sheria ya moja ya tatu(tusisahau pia kwa miaka 6 mshahara haijaongezwa) na hata wengi wa wanaokopesheke huishia kuchukua mkopo juu ya mkopo mwingine(top- up) na matokeo ni watu kupata vihela vidogo visivyokidhi mahitaji yao.
Mwisho, sheria ya mtumishi kutakiwa kubaki na moja ya tatu ya mshahara wake, nayo ipitiwe upya kwani haikuzingatia tofauti ya mishahara iliyopo baina ya watumishi na uhuru wa mtumishi kutumia mshahara wake kadri anayotoka.
Pia, kwakuwa mishahara serikalini ni midogo na haikidhi mahitaji, serikali iwaache watumishi kuamua ni namna gani watatumia mishahara yao kuendesha maisha yao.
Kumjali mtumishi sio kwa kumuwekea sheria ya kumlazimisha kubaki na moja ya tatu ya basic salary yake, bali ni kwa kuboresha masilahi yake( mtu miaka 6 mshahara ule ule halafu bado unampangia matumizi?).Haingii akilini.
CC: mwigulu nchemba