Serikali kupitia BoT, iruhusu watumishi wa umma wanaolipwa posho za mwezi kukopa kupitia posho zao

Mleta mada hujielewi kabisa mkopo Ni Kati ya mkopaji na mkopeshaji tu hakuna mtu wa tatu

Mwajiri au Benki kuu hawawezi kuingilia hiyo process

Kwa ulivyoandika unaonyesha umelenewa na madeni pesa unapeleka wapi? Unafanyia Nini Cha maana?
Wewe ndu huelewi lakini unajiona unaelewa sana. Mleta mada yuko sahihi, posho za chakula/vinywaji haziruhusiwi kukopewa Benki na mwajiri hatapitisha mkopo huo. Hakuna mkopo unatolewa na benki kwa mtumishi bila kuidhinishwa na Mwajiri hivyo kusema mkopo ni wa pande 2 pekee siyo sahihi.
 
Mshahara tuu unatosha . Wakikopea kila kitu wanaanza kuwa na tamaa na kuanza kutafuta rushwa ili waweze kuendesha maisha Yao
 
Acha ujinga were,unataka waishije? Kama mishahara imekopewa mpka 1 ya tatu,
 
Amenikera sana huyu bavicha,anataka wanajeshi waishi kama walimu? Maana walimu wanakopa benki na bado wanakopa mtaani wanaacha kadi.Matokeo yake wanaishi maisha ya hovyo sana.
 
mkuu posho/allowances zinaweza kusitishwa any time mambo yakiwa magumu, sasa unawezaje kukopa kupitia income ambayo haina uhakika kwamba mwakani itakuwepo?
 
Kimeuma! Wewe si huwa unajifanya mjanja kupinga wazalendo wa nchi hii
 
Kwanini uangaike na mkopo ikiwa una fedha zako PSSF au NSSF kwanini isitungwe sheria mtu awe na uwezo wa kuchukua nusu ya alichochangia akihitaji sio kusubiri mpaka akaribie kufa ndio apewe haki yake
 
Kikubwa unapaswa kuelewa historia ya utoaji wa mikopo Tanzania,
1-Mwanzoni kabisa watumishi walikuwa wanakopa karibu mshahara wote-Hii ilipelekea maisha magumu mno na malalamiko makubwa miongoni mwa watumishi wenyewe na kuipelekea serikali kuanzisha utaratibu wa 1/3 ya Basic pay ya mtumishi isiwe inakopesheka ili kuhakikisha mfanyakazi anakuwa na utulivu kazini nk.
2-Marupurupu hayapo guaranteed na sheria,hvyo mtumishi anaweza kuyapoteza wakati wowote ule katika utumishi wake-Sasa kama mtumishi alikopea hadi marupurubu na ikafika wakati akayapoteza itapelekea kuathiri sheria ya 1/3 ya Basic pay na hvyo kurudisha tatizo mwanzoni kabisa.
 
mkuu posho/allowances zinaweza kusitishwa any time mambo yakiwa magumu, sasa unawezaje kukopa kupitia income ambayo haina uhakika kwamba mwakani itakuwepo?
Hilo nalijua san
Kwanini uangaike na mkopo ikiwa una fedha zako PSSF au NSSF kwanini isitungwe sheria mtu awe na uwezo wa kuchukua nusu ya alichochangia akihitaji sio kusubiri mpaka akaribie kufa ndio apewe haki yake
Posho nazizungumzia hapa ni zile za kila mwezi tana ambazo ni sawa na mshahara wa mtu na sio zile za safari,vikao. Hizi nazoongelea zipo kwa baadhi ya taasisi na hutoka lila mwezi kwa wafanyakazi wote.

Kama unaweza kuchukulia mkopo wa muda mfupi(miezi 6 au 9) ukafanya mambo yako,shida iko wapi?

Tuacha kuishi kwa maziea. Hata salary advance ni ubunifu wa watu na unasaidia wengi.

Hilo PSSF na NSSSF pia watakupinga tu kwa hoja unataka wastaafu hela zao zianze kutumika kabla hawajastaafu.
 
Attack hoja yake na siyo maisha yake binafsi mkuu.
 
Swali la msingi la kujiuliza,Je, mtumishi akiamishwa ndani ya mwezi mmoja kwenda taasisi nyingine ya serikali ambayo haina marupurupu repercussion yake kwenye utaratibu wa 1/3 wa Basic pay kama take-home itakuweje?
 
Sasa hiyo moja ya tatu kwanini iwe ni kwa watumishi wote ili hali tofauti ya mishahara ni kubwa mno serikalini?

Mimi ndio maana nasema watanzania ni wavivu wa kufikiri na ni watu wa kuishi kwa kukariri na kukaririshwa.

Mfano, mtu mwenye basic ya shilingi 2,000,0000 au 1,500,0000, kwaninii abanwe na sheria moja na mtu mwenye basic ya shilingi 500,000 au shilingi 450,000?

Tuache uvivu wa kufikiri.
 
Umemwaga points sana chief
 
Hivi vitu ili upate majibu sahihi ni lazima ufikirie objectively kwa kujua historia ya 1/3 and etc,haikuja kirahisi-There is a logic behind it.
 
Swali la msingi la kujiuliza,Je, mtumishi akiamishwa ndani ya mwezi mmoja kwenda taasisi nyingine ya serikali ambayo haina marupurupu repercussion yake kwenye utaratibu wa 1/3 wa Basic pay kama take-home itakuweje?
Hii ndio hoja ya msingi umetoa ila kwenye mkataba wa mkopo hilo linaweza kuwekewa makubaliano na ukumbuke hii ni mikopo ya muda mfupi tu.
 
Hivi vitu ili upate majibu sahihi ni lazima ufikirie objectively kwa kujua historia ya 1/3 and etc,haikuja kirahisi-There is a logic behind it.
Hiyo moja ya tatu ni hoja mfu kabisa na haina uhalisia kwani mshahara huo unabaki kwenye makaratasi tu na ukitoka sio wa mtumishi bali unaenda kulipa madeni hivyo hilo lengo halifikiwi.
 
Hiyo moja ya tatu ni hoja mfu kabisa na haina uhalisia kwani mshahara huo unabaki kwenye makaratasi tu na ukitoka sio wa mtumishi bali unaenda kulipa madeni hivyo hilo lengo halifikiwi.
Watu walifanya research wakaja na mapendekezo ya 1/3 na ikawa acceptable na mabenki na wadau mbalimbali wakupigania haki za watumishi,leta sasa na wewe paper yako kui-move jamii kwenye mabadiliko ya hii sera zaid ya kuwa subjective.
 
Hiyo moja ya tatu ni hoja mfu kabisa na haina uhalisia kwani mshahara huo unabaki kwenye makaratasi tu na ukitoka sio wa mtumishi bali unaenda kulipa madeni hivyo hilo lengo halifikiwi.
Hakuna mahala popote hata kwenye biashara hapa duniani utakuta collateral ina thamani ya 100M alafu ikakopesheka kwa 100M kwenye taasisi halali za kifedha,where? Let's be practical
 
Watu walifanya research wakaja na mapendekezo ya 1/3 na ikawa acceptable na mabenki na wadau mbalimbali wakupigania haki za watumishi,leta sasa na wewe paper yako kui-move jamii kwenye mabadiliko ya hii sera zaid ya kuwa subjective.
Soma hii itakusaidia kupanua akili.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…