Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Serikali Kupitia (TAFORI) Ipo Tayari Kupokea Ushauri wa Tafiti za Miti ya Mikaratusi Ili Kupunguza Athari za Mazingira
"Kuna zaidi ya Species 500 za Miti ya Mikaratusi Duniani, Tanzania kupitia Taasisi ya Utafiti Misitu Nchini (TAFORI) imeruhusu aina 25 za Miti ya Mkaratusi ili kupata fursa mbalimbali zitokanazo na aina hii ya Miti ya Mkaratusi hasa kwenye viwanda vya mazao yaliyosindikwa. Serikali kupitia TAFORI inaendelea na Utafiti wa kina wa Mikaratusi ili kujua taarifa za kitaaluma na ushauri kuhusu athari za kimazingira. Baada ya tafiti kukamilika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii zitatoa elimu kwa wananchi kuhusu Miti ya Mikaratusi" - Mhe. Hamza Khamis Hamza Chilo, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
"Taarifa za kitaalamu zinaonyesha Miti ya Mikaratusi inatumia Lita 15 mpaka Lita 20 kwa siku kwa Mti mmoja. Je, Serikali iko tayari kuhudumia Miti kutengeneza Skimu Maalum za kumwagilia Miti wakati wakiendelea na mchakato wa kufanya utafiti?" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai
"Kwakuwa bado Serikali haina taarifa za utafiti wa athari za Miti ya Mikaratusi, Je, Serikali iko tayari kupokea tafiti za watu binafsi ambazo ziko nyingi zimefanyika kuhusu madhara na athari za Mti wa Mkaratusi ili ziweze kuzitumia kama tafiti rasmi za Serikali? - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai
"Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Mazingira tumegundua ipo baadhi ya Miti inatumia maji mengi mpaka kufikia kupunguza vyanzo vya Maji. Mpango aliotushauri Mbunge Saashisha Mafuwe wa kuandaa Skimu Maalum ipo katika Mipango ya Wizara na tunakwenda kuondoa changamoto hii, Serikali tunahimiza watu wapande Miti tofauti" - Mhe. Hamza Khamis Hamza Chilo, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
"Serikali ipo tayari kupokea tafiti kutoka Taasisi za Serikali, Taasisi binafsi ili kuondoa changamoto hii. Wizara nyingi tumekuwa tukipokea tafiti mbalimbali. Tunachotaka Tafiti zifuate utaratibu na zitoe mapendekezo Wizara ifanye nini. Kama Wizara tupo tayari kupokea tafiti" - Mhe. Hamza Khamis Hamza Chilo, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Your browser is not able to display this video.