Kadi za simu kwa vitambulisho
Maulid Ahmed
Daily News; Thursday,January 15, 2009 @20:01
WIZARAya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia inatarajia kupeleka bungeni Muswada wa Sheria ya Mawasiliano ambapo mtu atanunua kadi ya simu na kupata namba ya simu kwa kitambulisho, badala ya utaratibu holela unaotumika sasa.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alisema hayo jana wakati akielezea mafanikio ya Wizara yake kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Alisema muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa katika Mkutano ujao wa Bunge la Jamhuri utakaoanza mwishoni mwa mwezi huu. Sambamba na hilo, wizara hiyo inatarajia kuanzisha rejesta ili kubaini matumizi mabaya ya simu za mkononi yakiwamo ya watu kutukanana au kutishana.
Akizungumzia wingi wa minara ya simu, alisema, tumezishauri kampuni za simu zishirikiane kutumia minara kwa kila mtu kuweka antena yake katika mnara mmoja, hasa iliyo maeneo ya makazi ya watu; Vodacom na Zantel wameshaanza kushirikiana.
Alisema jumla ya watumiaji wa simu nchini hivi sasa ni 11,719,000 na kati yao 163,300 ni wa simu za mezani na 11,555,700 za mkononi. Hata hivyo alisema takwimu hizo zinatokana na kadi za simu zilizouzwa mpaka sasa.
Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wamefanikiwa kuondoa simu za kukoroga na kuanzisha huduma za simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya Code Division Multiple Access.
Alitaja mafanikio mengine kuwa ni kukamilisha ujenzi wa mitambo mipya ya kupitisha taarifa za intaneti katika manispaa za Arusha, Dar es Salaam na Mwanza. Ujenzi wa vituo vingine vya Dodoma na Zanzibar unatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha. Kadi