Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, ameagiza wataalamu wa wizara hiyo kufanya tathmini ya maduka ya kubadilisha fedha na kurejesha leseni kwa wenye vigezo ambao awali walifutiwa.
Katika mahojiano na Kituo cha Azam TV jana, Dk. Nchemba alisema kwa sasa wanafanya tathmini mpya.
“Tathmini kwa upande wa upatikanaji wa huduma hiyo kupitia benki ilishakamilika. Hatua inayofuata ni tathmini kwenye maduka binafsi ambayo na yenyewe yanaendelea kuratibiwa kadri ya vigezo vilivyowekwa na siku siyo nyingi mtaanza kuona yale yanayokidhi vigezo yataanza kutoa huduma,” alibainisha.
Alisema ameshakutana na kufanya mazungumzo na baadhi yao na amezipokea hoja zao na mojawapo walimwambia kuwa hiyo ni kazi yao, hivyo warudishiwe leseni.
"Tayari nimeshawaelekeza watu wangu wafanye tathmini ili wazirudishe, wakirudishwa kazini tutakusanya kodi, kwa hiyo hii ndiyo nimewaambia,” alisema.
Waziri Mwigulu alisema hoja ya pili waliyosema ni kuhusu mtaji uliowekwa umekuwa juu na ameielekeza timu yake ya wataalamu ifanye tathmini.
"Kitu ambacho ninataka kuwaomba Watanzania tuelewane vile vitu vinavyokuwa vya kisera ambavyo vina manufaa mapana ya nchi, ni vyema tukajifunza kukubaliana nayo kwa sababu pia tukiwa na nchi ikawa na utakatishaji wa fedha wa kiwango kikubwa au inayotumia fedha ya nchi nyingine inapunguza heshima ya uhuru wetu,” alisema.
VIGEZO
Alisema vigezo vitakuwapo kwa sababu awali kulikuwa na makosa kwenye uanzishaji wake katika baadhi ya maeneo.
“Hata vituo vya mafuta huwa inashauriwa umbali fulani hivi kama vinafuatana na kama vinatazamana, hata maduka yanatakiwa yampe urahisi yule mtumiaji kwa eneo.
“Ilenge shughuli zinazohitaji zaidi dola na fedha nyingine za kigeni kwa sababu maduka ya fedha za kigeni yasipothibitiwa, ni chanzo kimojawapo cha utakatishaji wa fedha," alisema.
Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo (CCM) aliliibua suala hilo wakati wa Bunge la Bajeti lililohitimishwa siku 10 zilizopita jijini Dodoma.
Gambo alikosoa uamuzi wa serikali kutumia nguvu kubwa wakati wa kuyafunga maduka hayo, akidai wafanyabiashara wengi walipokwa fedha zao na serikali.
Hata hivyo, Waziri Nchemba alipoulizwa kuhusu hoja hiyo wakati wa mahojiano jana, alisema ni suala la uchunguzi.
“Hakuna eneo ambalo jambo limefanyika bila hatua za kiuchunguzi, hatua za kiuchunguzi huwa zinaleta majawabu tofauti tofauti, kujibu kwa ujumla wake linaweza lisiwe jibu sahihi kwa maana hiyo lile ni jambo mahususi ambalo kama kuna eneo ambako kulikuwa na taratibu za kiwango hicho linatakiwa kuwa 'treated' kwa umahususi wake.
“Lakini, kwenye hoja ya jumla ni kwamba kulikuwapo na matatizo ya kisera, sehemu nyingine maduka yetu unakuta yamepangana yenyewe eneo moja.
“Sehemu nyingine unakuta fedha iliyopo kwenye maduka ni kubwa kuliko fedha iliyoko kwenye benki, madhara yake ni kushusha thamani ya fedha ya Tanzania, mnakuwa na nchi inayotumia fedha ya nchi nyingine," alifafanua.
Waziri Nchemba alisema ukiwa na maduka ya kubadilishia fedha kila baada ya nyumba moja na fedha zilizopo humo ni nyingi kuliko zilipo benki, hiyo inamaanisha nchi inatumia fedha za kigeni.
Source: IPP Media