Serikali kurudisha Ligi ya Muungano ili kuupa afya Muungano, yaunda kamati kutathmini gharama

Serikali kurudisha Ligi ya Muungano ili kuupa afya Muungano, yaunda kamati kutathmini gharama

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul akijibu swali Bungeni amesema Kamati imeundwa kufanya tathimini ya kurejesha Ligi ya Muungano ambayo inajumuisha timu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Waziri Gekul amesema “Tumekuwa na mazungumzo kati ya TFF, BMT na ZFF kwa afya ya muungano wetu tumekubaliana ligi kurudishwa hivi karibuni.”

Kipindi kile yalikuwa mashindano yenye tija na ushindani kwa maana bingwa alipata nafasi ya kuwakilisha Taifa kwenye Klabu bingwa ya Afrika.

Ila baada ya Zanzibar kupata nafasi yao huko CAF mashindano yakafa.

Hivyo yakirudi yatakuwa kama bonanza tu, na kujaza kalenda ya michezo.
Yawepo tu hata kama kipolitike.
 
Wanasiasa wanaendelea kuonyesha makucha yao. Kuna siku hawa watu wataturudishia vijiji vya ujamaa maana wameshaturudisha mfumo wa chama kimoja.
 
Napongeza yarudishe nakumbuka yalikuwa na msisimko sana.

Pia kulikuwa na kombe la AICC haya nayo yarudishwe yaliimarisha sana uhusiano wa nchi za EA
 
Hapa target clubs ni simba na yanga, sasa wakitaka matatizo walete fyoko kujifanya calendar zao zimebana, hili swala limekaa kisiasa zaidi

Nashauri libaki kombe la mapinduzi tuu linatosha
 
Mashindano ya kijinga yasio na tija labda km Zanzibar itaacha kushiriki mashindano ya caf
 
Kipindi kile yalikuwa mashindano yenye tija na ushindani kwa maana bingwa alipata nafasi ya kuwakilisha Taifa kwenye Klabu bingwa ya Afrika.

Ila baada ya Zanzibar kupata nafasi yao huko CAF mashindano yakafa.

Hivyo yakirudi yatakuwa kama bonanza tu, na kujaza kalenda ya michezo.
muhimu waangalie hz nafasi za timu huko caf.kwa sasa zanzibar 2 .bara 4
 
Kipindi kile yalikuwa mashindano yenye tija na ushindani kwa maana bingwa alipata nafasi ya kuwakilisha Taifa kwenye Klabu bingwa ya Afrika.

Ila baada ya Zanzibar kupata nafasi yao huko CAF mashindano yakafa.

Hivyo yakirudi yatakuwa kama bonanza tu, na kujaza kalenda ya michezo.
Labda kuwe na mechi moja tu baina ya bingwa wa NBC PL vs bingwa wa Zanzibar tena ifanyike kwa zamu, mwaka huu bara na mwaka ujao Zanzibar.

Vv
 
Ccm wanapenda sana kuingiza siasa kwenye kila kitu matokeo yake nchi iko nyuma karibu kwa kila kitu.
 
Back
Top Bottom