Serikali kusajili vibanda vyote vinavyoonesha sinema vimeshatambuliwa tayari

Serikali kusajili vibanda vyote vinavyoonesha sinema vimeshatambuliwa tayari

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Dodoma. Bodi ya Filamu Tanzania imeanza uhakiki wa vibanda vya kuonyeshea filamu maarufu vibanda umiza vilivyopo mtaani lengo ni kuvisajili na kuweka utaratibu wa undeshaji.

Pia wameunda Kamati maalum ya kuhamasisha Watanzania kurejesha utamaduni wa kuangalia filamu katika kumbi za sinema.

Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo, Dk Kiagho Kilonzo ameyasema hayo leo Jumanne Oktoba 4, 2022 wakati akielezea utekelezaji wa shughuli za bodi na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka 2022/2023.

Amesema hivi sasa Tanzania kuna kumbi tisa ambazo ziko katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Tanga na Dodoma na kwamba Serikali haiwezi kuhamasisha uwekezaji katika eneo hilo bila kuongeza idadi ya watu wanaokwenda kwenye kumbi hizo.

Amesema mapato ya wasanii yatatokana na uwepo wa kumbi hizo ambapo kwa programu ya sasa na asilimia 45 ya mapato yanayotokana na kumbi hizo yamekuwa yakienda kwa wasanii.

“Tumeishaanza kuvitambua. Na tayari timu yangu ipo kazini inapita kwa kushirikiana na maofisa utamaduni kujua kila mtaa kuna vibanda umiza vingapi na kuvisajili na baada ya hapo tutavipa utaratibu jinsi gani vinajiendesha,”alisema.

Aidha, Dk Kilonzo amesema kwa kupitia Kamati ya Kutetea Haki za Wasanii wamefanikiwa kurejesha Sh300 milioni kwa wasanii akiwemo marehemu King Majuto ambazo walidhulumiwa kutokana na mikataba mibovu.

Amesema pia bodi inataribu kamati maalumu ya kutetea haki za wasanii ambapo malalamiko 22 yamesuluhishwa huku nane yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema katika sekta ya filamu kumekuwa na mafanikio makubwa kwani nchi imeweza kutangazwa.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Kuna watu wanapenda kuharibu Hali ya hewa Kwa kweli,tizama bavicha walivyokuja mbiombio kushusha reply maji taka
 
Serikali kuvisajili vibanda umiza.

Chanzo: Mwananchi Online

Tunaacha Kusajili Migodi na Mbuga Bubu za Wanyama ili ziweze Kutuneemesha zaidi Watanzania Sisi tuko busy kutaka Kuvisajili Vibanda Umiza.

Huwezi kukuta Upuuzi huu nchini Rwanda na kuna Mambo yanatokea Tanzania kiasi kwamba hata ukiwa Umejumuika na Wageni kujitambulisha Wewe ni Mtanzania inakuwa ni Mtihani mzito.
 
Hakuna ataishi milele itabaki milima tu
 
Back
Top Bottom