Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SERIKALI KUTOA MUONGOZO WA KUAJIRI WANAOJITOLEA
Serikali imeeleza kuwa iko hatua za mwisho kukamilisha mwongozo utakaoangazia jinsi ya kuwaingiza katika mfumo watumishi wanaojitolea nchini.
Hayo yameelezwa, Jumatano, Januari 29, 2025, na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Lulindi (CCM), Issa Mchungahela.
Mchungahela amehoji Serikali inazungumziaje watumishi wanaojitolea katika kada mbalimbali, hususan ya elimu, ambako kuna watu waliojitolea kwa zaidi ya miaka 10.
Akijibu swali hilo, Sangu amesema jambo hilo limekuwa likizungumzwa mara kwa mara bungeni na kwamba Serikali iliahidi kulifanyia mchakato, ambao hivi sasa umefika katika hatua za mwisho.