Serikali kutoa ruzuku shule binafsi

Crystal field theory

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2014
Posts
940
Reaction score
401
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Serikali inaangalia iwezekano wa kuzipa ruzuku shule binafsi ili ziweze kujiendesha vizuri huku akizimwagia sifa shule za Tusiime kwa kuendelea kufanya vizuri kwa kutoa elimu bora na katika viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.

Alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki wakati alipozindua jengo la maabara za sayansi na maktaba ya shule hizo na mahafali ya tano ya kidato cha sita ambapo Membe alikuwa mgeni rasmi.

Alisema Serikali imegundua umuhimu huo wa kuzipa ruzuku na imeanza kuliangalia upya suala hilo kwani litasaidia shule binafsi kupunguza ada hivyo Watanzania wengi kupata fursa ya kupata elimu kwasababu gharama zinapopanda wazazi wamekuwa wakiumia.

Alisema nguvu ya uchumi wa gesi inaonesha kuwa Tanzania itakuwa na uwezo wa kifedha wa kutoa ruzuku kwa shule binafsi kama ilivyo kwa baadhi ya nchi duniani ambapo shule hizo hupewa ruzuku ya hadi asilimia 40.

Alisema kwa maendeleo ya wanafunzi kitaaluma shuleni hapo ni ushahidi tosha wa dhamira ya dhati waliyonayo Tusiime kama taasisi ya kutoa elimu bora kwa vijana wa kitanzania kwani wamekuwa wakifanya vyema katika mitihani mbalimbali ya kimkoa, kikanda na kitaifa.


Chanzo: HabariLeo
 
Angekuwa EL ndio mgeni mwaliko hapo tungeshasikia maCCM yanavyoweweseka!

On a serious note, mimi naamini ni wazo zuri kuzisaidia shule binafsi kama inavyofanya kwa huduma za afya. Wananchi ni walewale na ni wao pia wanaolipa kodi. Ingawa linahitaji umakini na uwazi katika kulitekeleza...lisije kuleta manung'uniko kama yale ya the famous "MoU".
 
jamani,mpaka uchaguzi upite tutasikia mengi ambayo hayaweza kutekelezeka.Matatizo ya shule tu ni mengi kwa sasa,hayajatafutiwa ufumbuzi,Hv hili la shule binafsi litawezekana?NAONA KAMA SIASA.
 
Hawa viongozi nadhani wanalazimishwa kusema maujinga yao ya kila siku au wako under influence au masikio yao hayasikii wanayoyasema. Binadamu katika hali ya kawaida anayeelewa situation ya government schools hawezi kusema haya.

Au ndio kujitengenezea mazingira ya kuvuna pesa kupitia shule zao vile washaona mwaka huu hawatapenya kirahisi.
 
hahaha!!! serikali inayoendeshwa kinadharia. maabara na maktaba zimewashinda kwenye shule za umma, iweje msitoe ruzuku kwa hizo shule muwache kuwasumbua wananchi!!?
 
Hapo ndo utajua kwamba hii serikali ni ya kisanii, kuhudumia shule zake tunaambiwa haina uwezo wa kutenga bajeti ya kutosha wakati inafikiria kuzipa ruzuku shule binafsi ambazo zinatoza ada mamilioni. Yaani inakusudia kuwasaidia wazazi wenye uwezo badala ya kuwasaidi wazazi wasio na uwezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…