benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa Bunge la 12 la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Katika mengi aliyoyazungumzia mimi nimefurashishwa na kitendo cha Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kulenga kutumia kutumia Shilingi Bilioni 150 kama ruzuku ya mbolea kwa mazao yote.
Ameeleza kuwa mfumo wa utoaji wa ruzuku utawalenga wazalishaji wa ndani lakini amepigilia msumari kuwa makampuni ambayo hayataungana na Serikali katika mfumo huu Serikali hatutosita kuwafutia leseni ya kuendesha biashara ya mboloea nchini.
Hatua hii ni mkombozi mkubwa kwa wananchi zaidi ya asilimia 70 ambao wanategemea kilimo hapa nchini. Hatua hii pamoja na ongezeko kubwa katika bajeti ya Kilimo 2022/23 itakwenda kupunguza mfumuko wa bei ya chakula nchini, kuongeza eneo la umwagiliaji, kuongeza upatikanaji wa ajira kwa vijana na wanawake katika kilimo zitakazofikia milioni 1 ifikapo mwaka 2025.