Serikali, kutoa taarifa kutetea wanyonge ni kosa Kisheria? Malisa kafanya kosa gani kupaza sauti ili walimu walipwe stahiki zao?

Serikali, kutoa taarifa kutetea wanyonge ni kosa Kisheria? Malisa kafanya kosa gani kupaza sauti ili walimu walipwe stahiki zao?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu kwema?

Serikali sasa huku mnapotupeleka kubaya, na ni uonevu wa wazi wazi kabisa. Yaani mtu anapaza sauti walimu wanadai stahiki zao badala mshughulikie malalamiko hayo mnaedna kumkamata aliyepaza sauti eti katoa taarifa bila kibali kwenye ukurasa wake wa Instagram!

Mtu anahitaji kibali kusema uonevu wa wengine au unaofanywa kwake? Katika inasemaje?

Haki ya Uhuru wa Mawazo
Uhuru wa
Maoni Sheria ya
1984 Na.15 ib.6

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Screenshot 2024-06-08 141717.png

Katiba imetoa haki hii ya kila mtu tutafuta na toa habari bila kujali mipaka ya nchi, sasa mmemkata Malisa kwa kosa gani? Au shule aliyotajwa ni ya Adolf Mkenda?
Yaani kwasababu masalahi yenu yanaguswa ndio mnakwenda kukamata mtu kwa sababu ya kijinga namna hiyo? Mmefanya nini kumshughulikia Adolf Mkenda ambaye anahusishwa na mambo lukuki mpaka sasa? Mfanyakazi aliyemuua Beatrice kwa kumchoma visu 25 alikuwa ni wake, mkapoteza kisayansi na kwa aibu yenu alifia mikononi mwa polisi.

Hizi aibu ndogo ndogo embu mziepuke, kwahiyo wananchi tunaolalamika kutwa kuchwa huduma mbovu, hatujalipwa stahiki zetu, barabara mbovu, nk, mtakuja kutukamata na kutufungulia kesi hizi za kipumbavu?

Halafu makaa kujitapa kila siku kuna uhuru wa kujieleza, kuna uhuru wa maoni, kuna utawala wa haki na sheria, SHAME ON YOU!

Ndio maana Makonda (japokuwa na yeye ni mpumbavu anayetatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ambazo nyienyie serikali na CCM hamjamchukulia hatua) anawapiga gepu, kila leo anaonesha udhaifu wa mahakama, utawala wa sheria na haki, lakini hata hamshituki, mmekaa tu utafikiri vichwa vimejaa maji.

Mnatia kinyaa!

====

Mwanaharakati na Mkurugenzi wa Taasisi ya GH Foundation, Godlisten Malisa, tayari ameripoti katika kituo cha Polisi Kati, mjini Moshi na kuanza kuhojiwa na maofisa kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Malisa alikamatwa Juni 6, 2024 muda mfupi baada ya kesi inayomkabili yeye na Meya wa zamani wa Ubongo, Boniface Jacob kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 8,2024 na mwanasheria wake, Hekima Mwasipu Malisa ameanza kuhojia saa 5:30 asubuhi na mpaka sasa anaendelea kuhojiwa na maofisa hao.

"Mwasipu amesema kwa sasa Malisa anahojiwa kuhusu tuhuma za kutoa taarifa bila kibali kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusu walimu waliokuwa wanasahihisha mitihani ya kidato cha nne Januari mwaka huu kutolipwa posho zao.

"Malisa ameitwa kuhojiwa na maofisa kutoka ofisi ya DCI kuhusu tuhuma za kutoa taarifa bila kibali kwenye akaunti yake ya Instagram, taarifa hiyo ni kuhusu walimu waliokuwa wanasahihisha mitihani ya form four mwaka huu mwezi Januari kutolipwa posho zao, "amesema Mwasipu.

Mwananchi
 
Wakuu kwema?

Serikali sasa huku mnapotupeleka kubaya, na ni uonevu wa wazi wazi kabisa. Yaani mtu anapaza sauti walimu wanadai stahiki zao badala mshughulikie malalamiko hayo mnaedna kumkamata aliyepaza sauti eti katoa taarifa bila kibali kwenye ukurasa wake wa Instagram!

Mtu anahitaji kibali kusema uonevu wa wengine au unaofanywa kwake? Katika inasemaje?

Haki ya Uhuru wa Mawazo
Uhuru wa
Maoni Sheria ya
1984 Na.15 ib.6

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

View attachment 3011854

Katiba imetoa haki hii ya kila mtu tutafuta na toa habari bila kujali mipaka ya nchi, sasa mmemkata Malisa kwa kosa gani? Au shule aliyotajwa ni ya Adolf Mkenda?
utashangaa WANA CCM jf wenye ubongo 0 wanashangilia
 
Masisiemu yatakuheshimu mda wote lkn sio mda uchaguzi ukikaribia....wanabadilika gafla wanakua mashetani
Kilichobaki tunachukua kanga zao na kofia na T-shirt ila kwenye sanduku la kura hawataamini.

Anachofanya sasahiv Tundu Lissu kinaweza kisiwashtue watu wengi ila kuna mbegu inapandwa taratibu.

Tutakula pesa zao na kwenye kura hawataamini.
Hayo si maneno yangu vijana wenyewe ndio wanasema hivyo. Mjumbe auwawi😀
 
Akipona saivi .

Aendelee na foundation yake. Mengine aachane nayo.
 
Kilichobaki tunachukua kanga zao na kofia na T-shirt ila kwenye sanduku la kura hawataamini.

Anachofanya sasahiv Tundu Lissu kinaweza kisiwashtue watu wengi ila kuna mbegu inapandwa taratibu.

Tutakula pesa zao na kwenye kura hawataamini.
Hayo si maneno yangu vijana wenyewe ndio wanasema hivyo. Mjumbe auwawi😀
Hii nchi ili ikombolewe wote wenye 36yrs++ wafe wote hawa watu walizembea sana waliruhusu uchafu mwingi sana ufanyike, wengi wapo kwenye serikalini wameshika nyadhifa za chini, kati na juu lakini wapo bize kujadili engine za watoto wa 2000
 
Tangulia kufa wewe
 
Back
Top Bottom